Ijumaa, 24 Novemba 2023

JAJI MKUU AKITAKA CHUO CHA UONGOZI WA MAHAKAMA LUSHOTO KUENDELEZA UTAMADUNI WA KUANDIKA HISTORIA ZA VIONGOZI WA MAHAKAMA

 Na Tiganya Vincent-Lushoto

 

Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amekitaka Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto kuendeleza na utamaduni wa kuandika historia za viongozi mbalimbali waliopita ili kusaidia kuhifadhi na kuonyesha michango yao katika kuutumikia Mhimili wa Mahakama nchini

 

Ametoa kauli hiyo leo tarehe 24 Novemba 2023 katika Mahafali ya 23 ya Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto ambapo jumla ya wanachuo 851 wamehitimu Kozi ya Sheria katika ngazi mbalimbali za Cheti.

 

Alisema Chuo cha Uongozi wa Mahakama kimejiongezea majukumu na kujipambanua kwenye eneo la uchapishaji wa vitabu  ikiwemo kile kinachoelezea Maisha na Ndoto ya Marehemu Jaji wa Mahakama ya Rufaa Robert Habesh Kisanga  kinachoitwa  A Dream Coming to Fruition: A Biography of Justice Robert Habesh Kisanga. 

 

Alisema kuwa zoezi walilokamilisha la uandishi wa Kitabu kinachoelezea historia ya Jaji  Kisanga ni kazi nzuri ambayo inapaswa kuendeleza kuandika hatika Historia za Viongozi wengine wa Mahakama ya Tanzania wakiwemo Majaji na Mahakimu ambao katika utekelezaji majukumu yao wamefanya makubwa ambayo yanapaswa kukumbukwa daima.

 

Mhe. Prof. Juma alisema machapisho mengine ni Utafiti wa utamaduni wa kimahakama (Exploring Judicial Culture in Tanzania) na mkusanyiko wa kesi za unyanyasaji wa kingono kwa watoto kwa nchini Tanzania pamoja na Ireland (A Compendium of Child Sexual Abuse Cases of Tanzania and Ireland)

 

Wakati huo huo Jaji Mkuu amewataka wahitimu wa Chuo hicho kuachana na fikira za kusubiria ajira katika sekta binafsi na za umma badala yake wafikirie kujijiari wenyewe katika sekta nyingine ambazo zinaweza kuwa hazina hata hazihusiani na kozi ya Sheria waliyosomea.

 

Alisema hatua hiyo itawasaidia katika kukabiriana na ukosefu wa ajira na hvyo kujipatia kipato kwa ajili ya maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.

 

Aidha Jaji Mkuu aliwataka Wahadhiri, Wanafunzi na watumishi wote katika Chuo hicho kujitahidi kupitia programu maalum ya mafunzo ili wapate ujuzi, umahiri wa kutoa huduma katika mazingira ya kidijitali. 

 

Alisema kikosi Kazi cha Mahakama kilichosimamiwa na Chuo hicho kilikamilisha Rasimu ya Mtaala wa kuendeshea mafunzo endelevu kwa watumishi wote wa Mahakama (BASIC DIGITAL SKILLS CURRICULUM FOR JUDICIARY STAFF).  

 

Mhe. Prof. Juma alisema ili mafunzo ya Mtaala huu yafanikiwe kwa watumishi wote wa Mahakama, Chuo Cha Uongozi wa Mahakama Lushoto lazima kiwe na uwezo wa kutoa haya mafunzo ambayo yatakiwezesha Chuo kutoa mafunzo yake kwa njia ya kidijitali. 

 

Katika hatua nyingine Jaji Mkuu wa Tanzania ameushukuru uongozi wa Wilaya na Wananchi wa Wilaya ya Lushoto kwa kutoa eneo ukubwa mita za mraba (square mita) 8,000 kwa ajili ya ujenzi wa Mahakama ya Kisasa ya Wilaya hiyo.

 

Alisema uongozi wa Mahakama ya Tanzania utafanyika kazi eneo hilo ili jengo litakalojengwa liwe Mahakama ya Wilaya na litumike kutoka mafunzo kwa Vitendo kwa wanachuo wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama cha Lushoto. 

 

Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto na Jaji wa Mahakama ya Rufaa ya Tanzana Mhe. Dkt. Paul Kihwelo alisema wamekamilisha uandaaji na uchapishaji wa kitabu kinachoelezea maisha ya Jaji wa Mahakama ya Rufaa Robert Habesh Kisanga  kinachoitwa  A Dream Coming to Fruition: A Biography of Justice Robert Habesh Kisanga ambacho uzinduzi wake utafanyika hivi karibuni.

 

Aidha Mkuu wa Chuo hicho alisema katika uboreshaji ufundishaji kwa wanacho wameandaa Jukwa ya kufundishia kwa njia ya Kieletroniki ambapo wako katika hatua za mwisho na sasa taratibu za kuwajengea uwezo Wataalamu wa namna ya kufundisha na kuandaa machapisho kwa njia ya mtandao.

 

Akimkaribisha Mgeni Rasmi Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto na Jaji wa Mahakama ya Rufaa Tanzania Mhe. Dkt. Gerald Ndika alisema kuwa Chuo hicho kimepata mafanikio makubwa katika utoaji wa Astashahada, Stashahada katika Sheria , uandaaji wa machapisho na uendeshaji wa warsha. 

 

Alisema Chuo kimejikita katika ufafiti ambao umesaidia kukithi matakwa ya wananchi na kimejika katika kinatoa elimu inaendana na mabadiliko ya wakati na kumudu ushindani

 

Katika mahafali hayo ya 23 jumla ya 336 wamekutunukiwa Astashahada ya Sheria , wanachuo 259 wa mwaka wa kwanza wametunikiwa Stashahada ya Sheria na wanachuo 272 wa mwaka wa pili wametunikiwa Stashahada ya Sheria.




 Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto na Jaji wa Mahakama ya Rufaa ya Tanzana Mhe. Dkt. Paul Kihwelo akitoa maelezo ya utangulizi leo tarehe 23 Novemba 2023 wakati wa Mahafali ya 23 ya. kuwatunukia Wahitimu 867 vyeti vya Sheria katika ngazi mbalimbali.


 


Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto na Jaji wa Mahakama ya Rufaa Tanzania Mhe. Dkt. Gerald Ndika akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi kwa ajili ya kuwahotubia wahitimu 867 wa kozi ya Sheria katika ngazi mbalimbali kwenye Mahafali ya 23 ya  Chuo hicho.



Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma  akitoa hotuba leo tarehe 24 Novemba 2023 katika Ukumbi wa Nyalalali kwenye Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto kabla ya wa kuwatunukia Wahitimu 867 vyeti vya Sheria katika ngazi mbalimbali.


 

Baadhi ya Wahitimu wa Astashahada ya Sheria kutoka Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto wakifuatilia hotuba ya Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (hayupo katika picha).


 



Baadhi ya Wahitimu wa Stahada ya Sheria mwaka wa kwanza kutoka Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto wakifuatilia hotuba ya Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (hayupo katika picha ) 



Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof . Ibrahim Hamis Juma (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na  Wajumbe wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Mahakama Lushoto mara baada ya kumalizika kwa Mahafali ya 23 ya Chuo hicho leo tarehe 23 Novemba 2023. 

 

Picha na Tiganya Vincent

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni