Ijumaa, 24 Novemba 2023

MAHAKAMA KUTANUA WIGO KUWAFIKIA WANANCHI

Na. Francisca Swai-Mahakama, Musoma.

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Musoma, Mhe. Fahamu Mtulya, amekabidhi vifaa vya kisasa vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), ikiwemo televisheni aina ya Moran yenye ukubwa wa inchi 65 katika Magereza ya Bunda na Tarime mkoani Mara. 

Akikabidhi vifaa hivyo kwa wakuu wa Magereza hayo, Mhe. Mtulya alisema, ‘‘Mahakama ya Tanzania imedhamiria kumfikia kila mwananchi pale alipo ili aweze kupata haki yake kwa wakati bila kujali mazingira aliyopo.’’

Jaji Mfawidhi alisema kuwa uwepo wa vifaa hivyo vya kisasa vyenye uwezo mkubwa, vitawezesha mashauri ya wafungwa na mahabusu kusikilizwa kwa wakati hata bila kufika mahakamani na kupata haki zao ndani ya muda sahihi. 

Naye Afisa TEHAMA wa Mahakama Kanda ya Musoma, Bw. Simon Lyova, alisema televisheni hizo zinauwezo wa kufanya kazi kama kompyuta au simu. 

Zina uwezo wa kuunganishwa kwa WiFi na Bluetooth, zina window 10 ni Android, zina kamera ya kuweza kuchukua picha au video ya mtu anayeitumia, zina kifaa cha sauti (microphone)….

“…zina uwezo wa kupokea taarifa kutoka televisheni nyingine (screen sharing), zina uwezo wa kufanya kazi kwa kugusa (touch), zinaweza kutumika kama ubao kuandikia kwa kalamu maalumu (white board), zinauwezo wa kuunganisha watumiaji zaidi ya mmoja (teleconference), alisema

Wakati huo huo, Jaji Mfawidhi, Kaimu Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Musoma Mhe. Erick Marley pamoja na Mtendaji wa Mahakama Kuu Musoma Bw. Festo Chonya, amefanya ukaguzi wa Mahakama mbalimbali ndani ya Kanda ya Musoma.

Katika ziara hiyo, Viongozi hao walitembelea baadhi ya majengo ya Mahakama yaliyofanyiwa ukarabati mkubwa pamoja na ujenzi kwa kutumia fedha za ndani na kuwasisitiza watumishi kuyatunza.

Pamoja na mambo mengine ,viongozi hao waliwasisitiza watumishi kudumisha umoja, upendo, mshikamano pamoja na kutimiza majukumu yao kwa uadilifu, weledi na uwajibikaji.


Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Musoma, Mhe. Fahamu Mtulya (kushoto), akimkabidhi Mkuu wa Gereza Msaidizi SP. Yusuph Rashidi Mkumbula, televisheni ya kisasa kwa ajili ya kusikiliza mashauri ya wafungwa na mahabusu katika Gereza la Bunda. Wengine ni viongozi mbalimbali wa Mahakama Kanda ya Musoma pamoja na maafisa wa Gereza Bunda.

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Musoma Mhe. Fahamu Mtulya (kushoto), akimkabidhi Mrakibu wa Magereza, Sebastian Dionis Askwary,  televisheni ya kisasa aina ya Moran kwa ajili ya kusikiliza mashauri ya wafungwa na mahabusu katika Gereza la Tarime. Wengine ni viongozi mbalimbali wa Mahakama Kanda ya Musoma pamoja na maafisa wa Gereza Tarime.


 Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Musoma, Mhe. Fahamu Mtulya (wa kwanza kulia) akisisitiza jambo wakati wa ukaguzi wa Mahakama ya Mwanzo Kiagata wilayani Butiama iliyojengwa upya kwa kutumia fedha za ndani.

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Musoma, Mhe. Fahamu Mtulya (katikati), Kaimu Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Musoma, Mhe. Erick Marley (wa tatu kushoto), Mtendaji wa Mahakama Kuu Musoma, Bw. Festo Chonya (wa tatu kulia), Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya ya Butiama Mhe. Judith Semkiwa (wa pili kushoto) Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Mwanzo Kiagata, Mhe. Kennedy Mwaikambo (wa kwanza kushoto), Afisa Tawala Mahakama ya Wilaya Butiama Bi. Teckla Patrick (wa pili kulia) na Mlinzi wa Mahakama ya Mwanzo Kiagata Bw. Boniphace Kanukanu (wa kwanza kulia), wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya jengo la Mahakama ya Mwanzo Kiagata iliyojengwa upya kwa kutumia fedha za ndani.

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Musoma Mhe. Fahamu Mtulya (wa pili kushoto) akisisitiza jambo wakati wa ukaguzi Mahakama ya Mwanzo Kenkombyo Wilayani Bunda,  iliyofanyiwa ukarabati mkubwa kwa kutumia fedha za ndani.

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Musoma, Mhe. Fahamu Mtulya (katikati), Kaimu Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Musoma Mhe. Erick Marley (wa tatu kushoto), Mtendaji wa Mahakama Kuu Musoma Bw. Festo Chonya (wa tatu kulia), Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya ya Bunda Mhe. Mulokozi Kamuntu (wa kwanza kushoto) Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Mwanzo Kenkombyo Mhe. Victoria Gambamala (wa pili kushoto), Afisa Utumishi Mahakama ya Wilaya Bunda Bi. Rose Millinga (wa pili kulia) na Msaidizi wa Kumbukumbu Mahakama ya Mwanzo Kenkombyo Bi. Tabu Ungura (wa kwanza kulia), wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya jengo la Mahakama ya Mwanzo Kenkombyo lililo fanyiwa ukarabati mkubwa kwa kutumia fedha za ndani.

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Musoma, Mhe. Fahamu Mtulya (katikati), Kaimu Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Musoma Mhe. Erick Marley (wa nne kulia), Mtendaji wa Mahakama Kuu Musoma Bw. Festo Chonya (wa nne kushoto), Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya ya Bunda Mhe. Mulokozi Kamuntu (wa tatu kulia), Afisa Utumishi Mahakama ya Wilaya Bunda Bi. Rose Millinga (wa tatu kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja baada ya ukaguzi wa Mahakama ya Wilaya Bunda.

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya MusomaMhe. Fahamu Mtulya (katikati), Kaimu Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Musoma Mhe. Erick Marley (wa pili kushoto), Mtendaji wa Mahakama Kuu Musoma Bw. Festo Chonya (wa pili kulia), Kaimu Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya ya Rorya Mhe. Julius Sisa (wa kwanza kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja baada ya ukaguzi wa Mahakama ya Wilaya Rorya.

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Musoma Mhe. Fahamu Mtulya (katikati) akiongea na watumishi wa Mahakama ya Wilaya na Mahakama ya Mwanzo Tarime Mjini (hawako pichani), wakati wa kikao cha ukaguzi wa Mahakama Wilayani Tarime.

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Musoma Mhe. Fahamu Mtulya (katikati), akifurahia mazingira na ukuaji wa miti (haionekani pichani) wakati wa ukaguzi wa Mahakama ya Mwanzo Natta iliyoko Serengeti.

(Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dar es Salaam)

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni