Jumapili, 26 Novemba 2023

MAHAKAMA YA TANZANIA KUSHIRIKIANA NA TAASISI ZINGINE KUTOA ELIMU MASUALA YA TEHAMA

Na. Evelina Odemba – Mahakama, Morogoro

 

Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabrieli amesema kuwa Mahakama ipo tayari kushiriana na Taasisi zingine kubadilishana uzoefu wa matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ili kuepuka gharama za uendeshaji  na utoaji huduma. 

 

Prof. Elisante aliyasema hayo tarehe 22 Novemba, 2023 wakati akitoa neno la hamasa kwenye hafla iliyowakutanisha Aluminai waliosoma Chuo Kikuu Mzumbe kilichopo mkoani hapa.


Hafla hiyo ilihudhuliwa na Viongozi mbalimbali, akiwemo Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia,Mhe. Prof. Adolf Mkenda, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Adam Malima, Viongozi wa Chuo Kikuu Mzumbe, Viongozi wa idara mbalimbali waliosoma chuoni hapo pamoja na wanafunzi waliohitimu ambao walikuwa wanapokelewa rasmi katika umoja huo.

 

Prof. Ole Gabriel alielezea mapinduzi makubwa yaliyofanywa na Mahakama ya Tanzania upande wa matumizi ya TEHAMA na kusema kuwa kwa sasa Majaji na Mahakimu wanaweza kusikiliza kesi kwa njia ya mtandao wakiwa wamekaa ofisini na kuunganishwa na wadaawa wakiwa mahali popote.

 

Sisi Mahakama ni Taasisi ambayo imejiimalisha katika matumizi ya TEHAMA, Majaji na Mahakimu wanaweza kusikiliza kesi kutokea Mkoa aliopo, haina haja ya kwenda Mbeya au Kataviataunganishwa kwa mtandao na kazi itaendelea…

 

 “Tupo tayari kubadilishana uzoefu huna Taasisi nyingine. Mfano, Mkufunzi anaweza kuwa yupo hapa anafundisha, vyuo vingine vinaweza kuunganishwa kwa njia ya mtandao kufuatilia kinachojiri hapa na hii itapunguza mzigo wa kutafuta wataalamu wengi, alisema.

 

Suala hilo lilipokelewa na kuungwa mkono na Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolijia aliyekuwa mgeni rasmi ambaye alitolea mfano kuwa miaka ya nyuma wakati wa kipindi cha Uviko-19 waliwahi kutumia TEHAMA kutoa huku Mkufunzi akiwa Accra Ghana na wanafunzi wanafuatilia kutoka mataifa mengine yaliyokuwa yamejiunga

 

Alichosema Prof. Ole Gabriel hapa ni lazima tukifanyikazi na kuongeza matumizi ya TEHAMA, hivyo tunalipokea kwa mikono miwili, ni suala ambalo limefanyika ndani ya Afrika itakuwa ajabu ndani ya Nchi tushindwe, naomba tulipokee na kulifanyia kazi,” alisema.

 


Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Gabriel akizungumza wakati wa hafla ya kuchangia ujenzi wa Hostel za wanafunzi wa kike katika Chuo Kikuu Mzumbe, Kampasi ya Mbeya

Mgeni rasmi ambaye ni Waziri wa Elimu, Sayansi na TeknolojiaMhe. Prof. Adolf Mkenda akizungumza wakati wa hafla hiyo.  


 Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Adam Malima akizungumza wakati wa hafla hiyo.

 

Meza Kuu ikiimba wimbo wa Taifa kabla ya kuanza rasmi kwa hafla hiyo.  Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel akiteta jambo na Rais wa  Convocation CPA Ludovic Uttoh wakati wa hafla.

 

Sehemu ya watumishi wa Chuo Kikuu Mzumbe  iliyoshiriki hafla hiyo.


(Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dar es Salaam) 

 

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni