Alhamisi, 16 Novemba 2023

UJUMBE MAHAKAMA YA TANZANIA WAKUTANA NA RAIS WA MAHAKAMA YA WILAYA VILNIUS

Na Tiganya Vincent,Vilnius -Lithuania

Ujumbe wa Mahakama ya Tanzania ukiongozwa na Mtendaji Mkuu, Prof. Elisante Ole Gabriel jana tarehe 15 Novemba 2023 ulikutana na Rais wa Mahakama ya Wilaya ya Mji wa Vilnius nchini Lithuania, Mhe. Viktorija Šelmienė kwa ajili ya kubadilisha uzoefu katika maeneo mbalimbali ya utoaji haki  kwa pande zote mbili.

Akizungumza mara baada ya kuwasili katika Mahakama hiyo, Mtendaji Mkuu Mahakama ya Tanzania, Prof. Ole Gabriel alisema ziara  hiyo imekuwa na manufaa kwa pande zote katika kufungua ukurasa wa kushirikiana katika kuboresha utoaji haki kwa wananchi wa Nchi hizo mbili.

Prof. Ole Gabriel aliwashukuru kwa mapokezi mazuri na kuwakaribisha Tanzania kwa ajili ya kuongeza ushirikiano zaidi pamoja na kubadilishana uzoefu katika kuboresha eneo la utoaji haki kwa wananchi.

Naye, Rais wa Mahakama hiyo ambaye pia ni Jaji anayejikita na kubobea katika mashauri ya Jinai (specialization in Criminal cases), Mhe. Viktorija Šelmienė alisema mfumo wa uendeshaji wa mashauri nchini humo unawagawa Majaji katika maeneo mawili ya wanaojihusisha na mashauri ya Jinai na wale wanaoshughulikia mashauri ya madai.

Alisema kwa Majaji wanaojihusisha na mashauri ya Jinai hawaruhusiwi kusikiliza na kuendesha mashauri yanayohusu madai na wale na wa madai vilevile hawapaswi kusikiliza mashauri ya Jinai.

Mhe. Viktorija alisema Nchi hiyo imekuwa na Majaji wengi wanawake ukilinganisha na wanaume, huku akibainisha kuwa, wanawake wamekuwa wakifanya vizuri katika mitihani ya kuomba kufanya kazi ya Ujaji na wamekuwa wakisifika kwa uchapaji kazi kwa bidii bila kujali maslahi makubwa.

Aliongeza wanaume wengi katika Nchi hiyo waliosomea Sheria wamekuwa wakitaka kazi ya Uwakili na nyinginezo ambazo wanalipwa maslahi makubwa.

Kadhalika, Mhe. Viktorija alisema kuwa, katika Nchi hiyo utambulisho wa mtoto katika shauri haufichi bali kuna Taasisi ambayo iko maalum kulinda haki za Watoto ambao ni waathirika.

Mhe. Viktorija alisema vifaa vilivyowekwa kama vile Kamera, kinasa sauti havionekani kwa mtoto na husaidia kwenye chumba cha pili kushuhudia maelezo ya mtoto bila hata kujua kuwa watu wanasikiliza maelezo yake.

Mtendaji Mkuu Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel (kushuto) akisamiliana na Rais wa Mahakama ya Wilaya ya Mji wa Vilnius nchini Lithuania, Mhe. Viktorija Šelmienė (kulia) mara baada ya kuwasili katika Mahakama hiyo jana tarehe 15 Novemba 2023 kwa ajili ya ziara ya mafunzo.

Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Angelo Rumisha (kushoto) akisamiliana na Rais wa Mahakama ya Wilaya ya Mji wa Vilnius nchini Lithuania, Mhe. Viktorija Šelmienė (kulia) mara baada ya kuwasili katika Mahakama hiyo jana tarehe 15 Novemba 2023 kwa ajili ya ziara ya mafunzo. Katikati ni Mtendaji Mkuu Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel na wa kwanza  kushoto ni Naibu Msajili Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Elimo Massawe.


Rais wa Mahakama ya Wilaya ya Mji wa Vilnius nchini Lithuania,  Mhe. Viktorija Šelmienė (kushoto) akitoa maelezo kwa ujumbe wa Mahakama ya Tanzania mara baada ya kuwasili katika Mahakama hiyo kwa ziara ya mafunzo .

Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel (kushuto) na Rais wa Mahakama ya Wilaya ya Mji wa Vilnius nchini Lithuania Mhe. Viktorija Šelmienė (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa ziara ya mafunzo ya kubadilishana uzoefu.

Mtendaji Mkuu Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel (kushuto), Rais wa Mahakama ya Wilaya ya Mji wa Vilnius nchini Lithuania, Mhe. Viktorija Šelmienė (katikati) na Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Angelo Rumisha (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa ziara ya mafunzo ya kubadilishana uzoefu wa utoaji haki katika Mahakama hiyo.

Picha ya pamoja kati ya Rais wa Mahakama ya Wilaya ya Mji wa Vilnius nchini Lithuania, Mhe. Viktorija Šelmienė  (wa tano kulia). Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Angelo Rumisha (wa nne kutoka kulia), Mtendaji Mkuu Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel (wa saba kushoto) pamoja na Maafisa wengine walioambatana na Mtendaji Mkuu.
Rais wa Mahakama ya Wilaya ya Mji wa Vilnius nchini Lithuania,  Mhe. Viktorija Šelmienė (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Angelo Rumisha (pili kutoka kulia), Mtendaji Mkuu Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel (wa pili kushoto), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Mhe. Jenifa Omolo (wa kwanza kushoto) na Mwakilishi wa Benki ya Dunia, Bw. Benjamin Mtesigwa (wa kwanza kulia).

(Picha na Tiganya Vincent)


(Habari hii imehaririwa na Mary Gwera, Mahakama-Dodoma)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni