Jumatatu, 13 Novemba 2023

MAJAJI MAHAKAMA YA RUFANI WAACHA ALAMA MUSOMA

Na. Francisca Swai-Mahakama Kuu, Musoma.

Jopo la Majaji watatu ambalo lipo mjini hapa kwa ajili ya kikao cha Mahakama ya Rufani limeacha alama Kanda ya Musoma baada ya kupanda miti mbalimbali kwenye maeneo yanayozunguka katika jingo la Mahakama Kuu ya Tanzania.

Majaji hao, Mhe. Mwanaisha Kwariko (Mwenyekiti), Mhe. Zephrine Galeba na Mhe. Dkt. Paul Kihwelo wamepanda miti katika bustani ya miti ya matunda iliyoko katika mazingira ya Mahakama hiyo.

Zoezi hilo la upandaji wa miti limefanywa kama kumbukumbu nzuri ya wao kutembelea Mahakama hiyo yenye mandhari nzuri na ya kuvutia na pia kuendeleza jitihada zinazofanywa na uongozi wa Mahakama hiyo katika utunzaji wa mazingira.

Jopo la Majaji hao wa Mahakama ya Rufani wameupongeza uongozi wa Mahakama Kuu Musoma pamoja na watumishi wote kwa namna wanavyotunza mazingira na wanavyofanya kazi kwa ushirikiano, upendo na umoja.

Viongozi hao wamewaasa watumishi kuendelea kufanya kazi katika misingi ya uadilifu, weledi na uwajibikaji.


Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Mwanaisha Kwariko (juu na chini) akipanda miti ya matunda (passion na stafeli) katika bustani ya miti ya matunda iliyoko Mahakama Kuu Musoma.

 

Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Zephrine Galeba akipanda mti wa Mdodoma katika bustani ya miti ya matunda iliyoko Mahakama Kuu Musoma.

Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Dkt. Paul Kihwelo akipanda mti wa matunda (Muembe) katika bustani ya miti ya matunda iliyoko Mahakama Kuu Musoma.



 

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Musoma, Mhe. Fahamu Mtulya akipanda mti wa matunda (Mchungwa) katika bustani ya miti ya matunda iliyoko Mahakama Kuu Musoma.



 

Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Musoma, Mhe. Marlin Komba akipanda mti wa matunda (Parachichi) katika bustani ya miti ya matunda iliyoko Mahakama Kuu Musoma.

Majaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Mwanaisha Kwariko (wa pili kushoto), Mhe. Zephrine Galeba (wa kwanza kushoto) na Mhe.  Dkt. Paul Kihwelo (wa tatu kushoto) wakitoa shukrani zao na pongezi kwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Musoma, Mhe. Fahamu Mtulya (wa nne kushoto), Mhe. Marlin Komba (wa tatu kulia), Mtendaji wa Mahakama Kuu Musoma, Bw. Festo Chonya (wa pili kulia) na Kaimu Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Musoma, Mhe. Aristida Tarimo (wa kwanza kulia) baada ya zoezi la upandaji wa miti katika bustani ya Mahakama Kuu Musoma.

(Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dar es Salaam)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni