Jumatatu, 13 Novemba 2023

PAZENI SAUTI KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA: JAJI SEHEL

Na. Stephen kapiga - Mahakama Mwanza.

Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA) na Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania Mhe. Barke Sehel amewasihi wanachama wa Chama hicho kuhakikisha kuwa kila mara wanapaza sauti na kuhakikisha kuwa wanapinga matendo yote ya ukatili wa kijinsia ambayo yamekuwa yakishamili katika jamii.

Akizungumza na wananachama wa Chama hicho hivi karibuni jijini Mwanza Jaji Sehel alitumia fursa hiyo alitoa mrejesho kwa sehemu ya wanachama wa Chama hicho wanaofanya kazi katika Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki jijini Mwanza juu ya kikao cha uchaguzi wa viongozi wa Chama hicho kitaifa uliofanyika jijini Tanga mnamo tarehe 17 Januari, 2023 na kufanikiwa kuchagulia kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho kwa kipindi cha miaka miwili pamoja na kamati tendaji yenye jumla ya wajumbe sita (6).

“Nawasihi sana mtumie kila nafasi mnayopata kuweza kupaza sauti zenu katika kukema ukatili huu wa kijinsia mabao unakuja kwa kasi hapa nchini.Mnapokuwa mkitoa maamuzi yenu msisite kuzungumza juu ya swala hili pia. Andikeni Makala mbalimbali ambzo zitaelimisha Jamii juu ya swala hili, pia tafuteni nafasi katika vyombo mbalimbali vya Habari kuweza kufikisha ujumbe kwa jamii juu ya masuala ya ukatili wa kinjinsia.”alisisitiza Mhe. Sehel. 

Jaji Sehel alisema kuwa, kumekuwa na matukio mengi ya unyanyasaji wa kijinsia hasa kwa njia ya mitandao ya simu au “social media” na hivyo kuwafanya wahanga wengi wa matukio hayo kufikia hatua ya kufanya maamuzi mabaya ikiwemo kujidhuru au kujiua.

“kwa sasa teknolojia inakua kwa kasi sana, watoto wengi wameingia kwenye matumizi ya simu na hapo ndipo wale wenye nia mbaya hufanya mawindo yao kwa kufanya unyanyasaji mitandaoni “cyber bullying” kwa watoto hao kwani wengi wao huangukia kwenye mikono ya wadukuzi “hackers” na kuchukulia kama faida kwao na hivyo watoto hawa au vijana hawa hukumbwa na msongo “stress” au kujiua kabisa kutoka na hali inayowapata baada ya kuwa wamefanyiwa unyanyasi mitandaoni “cyber bullying” huko mitandaoni”, alisema Mhe. Sehel

Aidha, Mhe. Sehel aliwakumbusha wananchama hao kuhusu siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ambao maadhimisho yake yataanza kuanzia tarehe 25 Novemba, 2023 na kufika tamati mnamo tarehe 10 Desemba, 2023 ambayo yatabebwa na kaulimbiu isemayo “Wekeza kuzuia ukatili wa kijinsia”, ikiwa mkoa wa Mwanza umepanga kufanya Mahakama ya mfano ya kupinga ukatili wa kijinsia “Moot Court” ambayo itafanyika siku ya tarehe 2 Disemba 2023 katika Chou cha Mtakatifu Augustino SAUT Mwanza na Mgeni Rasmi anategemewa kuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw. Amos Makalla.

Mhe. Sehel aliema kuwa, mpaka sasa Mpango Mkakati wa Chama hicho umeshaandaliwa na timu ya watalaam wa ndani na unategemewa kuwa tayari ifikapo tarehe 18 Novemba, 2023 chama kinatarajia kufanya kikao kwa ajili ya kupitisha rasimu wa Mpango Mkakati huo na wajumbe wote watatumiwa kwa ajili ya kupitia kwa njia ya mawasiliano iliyokubalika katika Chama hicho.

Katika kikao hicho Mhe. Sehel aliwakumbusha wanachama wa TAWJA kujiandaa na kufanya maandalizi kabambe ya kuelekea wiki ya sheria mwaka 2024 yenye kauli mbiu isemayo kuwa, Umuhimu wa Dhana ya Haki Jinai kwa ustawi wa taifa, nafasi ya Mahakama, Wadau kwa ajili ya kuhuhisha mfumo wa haki Jinai na kuwa tayari kujitolea kwenye maeneo ambayo wanachama hao wanauzoefu kwa ajili ya kuweza kusaidia wanawake katika jamii inayowazunguka.

Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA) na Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania Mhe. Barke Sehel akizungumza na sehemu ya wanachama wa chama hicho (hawapo pichani) wanaofanya kazi katika Mahakama zilizopo Mwanza Mjini. Wengine ni Jaji wa Rufani ya Tanzania Mhe. Dkt. Mary Levira (kulia) na kushoto ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mwanza Mhe. Irene Musokwa katika kikao cha mrejesho na wanachama hao kilichofanyika katika Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki jijini Mwanza.



Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA) na Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania Mhe. Barke Sehel akizungumza na sehemu ya wanachama wa chama hicho (hawapo pichani) wanaofanya kazi katika Mahakama zilizopo Mwanza Mjini. Wengine ni Jaji wa Rufani ya Tanzania Mhe. Dkt. Mary Levira (kulia) na kushoto ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mwanza Mhe. Irene Musokwa katika kikao cha mrejesho na wanachama hao kilichofanyika katika Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki jijini Mwanza

(Habari Hii Imehaririwa na Innocent Kansha - Mahakama)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni