Jumatatu, 11 Desemba 2023

MAHAKIMU MOROGORO WAPIGWA MSASA ELIMU YA JOPRAS

Na Evelina Odemba – Mahakama Morogoro

 

Mahakimu wa Mahakama ya Tanzania katika Kanda ya Morogoro hivi karibuni walipewa elimu juu ya kujaza taarifa za kiutendaji kazi kupitia mfumo wa upimaji kazi kwa Mahakimu (JOPRAS).

 

Mafunzo hayo yaliyoratibiwa na ofisi ya Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Morogoro, Mhe. Augustina Mbando yalifunguliwa na Jaji Mfawidhi, Mhe. Latifa Mansoor ambaye pia alikuwa mshiriki.

 

Elimu hiyo ilitolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro, Mhe. Livin Lyakinana kupitia mtandao, yaani Video Conference, na washiriki wote walipata elimu wakiwa katika vituo vyao.

 

Awali, wakati akitoa mafunzo hayo, Mhe. Lyakinana alieleza kuwa ni vyema kuzingatia uwajibikaji ili taarifa sahihi ziweze kujazwa.

 

Aliwapitisha hatua kwa hatua kwenye vipengele vya ujazaji taarifa hizo muhimu katika upimaji wa uwajibikaji wa Majaji na Mahakimu nchini.

 

Naye, Jaji Mfawidhi, wakati akifunga mafunzo hayo aliwasisitiza Mahakimu kuzingatia kilichofundishwa ili takwimu sahihi ziweze kupatikana.

 

“Niwashukuru wote mlioshiriki kikao hiki kikamilifu na rai yangu kwa wote tuzingatie kile kilichofundishwa ili takwimu sahihi ziweze kupatikana, tunashukuru sana kwa mafunzo haya kwa kuwa yametupatia msingi mzuri,” alieleza Mhe. Mansoor.

 

JOPRAS ni fomu zinazotumika kupima utendaji kazi wa Mahakimu na Majaji, ikiwemo kupangiwa na kusikiliza mashauri na kuyatolea maamuzi kwa kuzingatia idadi ya mashauri. Fomu hizi hujazwa kila ifikapo mwisho wa mwezi.

 


Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Morogoro, Mhe. Latifa Mansoor akifuatilia mafunzo ya ujazaji wa taarifa za JOPRAS kwa njia ya mtandao akiwa ofisini kwake.

 

Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Morogoro, Mhe. Augustina Mmbando akiratibu wakati wa mafunzo hayo.

 

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro, Mhe. Livin Lyakinana akitoa elimu ya ujazaji wa taarifa za JOPRAS kupitia mtandao.

 


Mkutano ukiendelea kupitia mtandao kama inavyoonekeana kwenye runinga iliyopo ndani ya Chumba cha kufanyia mkutano.


 

Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Mvomero, Mhe. Asha Waziri akifuatilia mafunzo kwa njia ya mtandao.

 


Kushoto ni muwezeshaji Mhe. Living Lyakinana akitoa elimu, kulia ni Naibu Msajili, Mhe. Augustina Mmbando akifuatilia ndani ya chumba cha mkutano kwa njia ya mtandao.

 


Mkutano ukiendelea.


 


Mahakimu (juu na chini) wakifuatilia mafunzo hayo huku wakiwa ndani ya ofisi zao.



Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dar es Salaam.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni