Na. Tawani Salum, Mahakama-Mwanza
Bodi ya Mhe. Jaji Mkuu wa Mahakama ya
Tanzania ya Udhamini wa Taarifa ya Juzuu la Sheria Tanzania (Tanzania Law
Reports) imekutana jijini Mwanza hivi karibuni na kufanya uchambuzi wa maamuzi
ya Juzuu la Mwaka 2023 (TLR 2023) baada ya kukamilisha Juzuu la Mwaka 2021 na 2022
(TLRs 2021/2022) katika hoteli ya Aden Palace iliyopo jijini Mwanza ikiwa na lengo
la ifikapo mwanzoni mwa Mwezi Januari Mwaka 2024 kukamilisha uchapaji wa Juzuu la
Sheria kwa miaka yote mitatu.
Akizungumza katika kikao cha Bodi hiyo, kilichochoanza kufanyika kuanzia tarehe 18 disemba, 2023 hadi tarehe 20 disemba,2023 Jijini Mwanza, Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania, Mhe. Jacobs Mwambegele alisema kuwa Juzuu la Mwaka 2021 na 2022 tayari limewasilishwa kwa Mzabuni kwa hatua ya upangaji wa juzuu (typesetting) na uchapaji.
“Ni mpango wa Bodi hii kuhakikisha kuwa inamaliza kuchambua Taarifa za Juzuu la
Sheria la Mwaka 2023 ifikapo mwezi wa Januari Mwaka 2024 ili hatua za
uchapaji zianze mapema na kukamilika kwa wakati na kuongeza wigo wa upatikanaji
wa rejea za maamuzi hayo.,” alisema Mhe. Jaji Mwambegele.
Naye Mratibu wa Bodi hiyo, Mhe. Kifungu
Mrisho Kariho ambaye ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Tanzania, alisema kuwa
Bodi hiyo imedhamiria kutoa Juzuu zote kwa mkupuo kwa kuwa tayari Bodi
imefanyia kazi uchambuzi wa maamuzi yote kwa miaka ya 2021 na 2023 na
kuwasilisha kwa mzabuni tayari kwa hatua ya uchapaji.
“Tunatarijia kuwa kuanzia Mwaka 2024 Bodi
hii itakuwa utaratibu wa kutoa Taarifa za Juzuu la Sheria kwa kila baada ya
Miezi sita katika Mwaka na baadaye tutaanza utaratibu wa kutoa taarifa kila
baada ya Miezi mitatu kwa mwaka husika.” Aliongeza Mhe Kariho
Bodi hiyo ina jumla ya Wajumbe 11,
ambao ni waheshimiwa Majaji kutoka Mahakama ya Rufani ya Tanzania, waheshimiwa Majaji
wa Mahakama Kuu ya Tanzania Bara, Wawakilishi kutoka Ofisi ya Mwanasheria
Mkuu Tanzania Bara na Zanzibar, Wawakilishi kutoka Vyama vya Mawakili Tanzania
Bara na Zanzibar, Katibu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mratibu wa Bodi
hiyo kutoka Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania.
Wajumbe wa Bodi ya Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania ya Udhamini wa taarifa ya Juzuu la sheria Tanzania wakiwa katika picha ya Pamoja wakiongozwa na Mwenyekiti wa bodi hiyo ambaye pia ni Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania Mhe. Jacobs Mwambegele(aliyeketi katikakati) na kushoto kwake ni Profesa Hamduni Ismail Majamba wakiwa Pamoja na wa wajumbe wengine wanaounda bodi hiyo iliyokutana hivi karibuni Jijini mwanza kwa ajili ya kujadili na kuandaa Juzuu ya taarifa ya sheria Tanzania ya mwaka 2023.
Wajumbe wa Bodi ya
Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania ya Udhamini wa taarifa ya Juzuu la sheria
Tanzania wakiwa katika kikao cha uandaaji wa Juzuu ya sheria za Tanzania za
mwaka 2023 kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Tanganyika ndani ya hotel ya
Aden Palace Jijini mwanza kikao kilichoongozwa na jaji wa Mahakama ya Rufani ya
Tanzania ambaye ndiye Mwenyekiti wa bodi hiyo Mhe.Jacobs Mwambelege.
Katibu wa Bodi ya
Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania ya Udhamini wa taarifa ya Juzuu la sheria
Tanzania Profesa Hamud Ismail Majamba akielezea jambo kwa wajumbe wa bodi hiyo (hawapo
pichani) wakati wa majadiliano juu ya uandaaji wa Juzuu ya sheria za Tanzania
kwa mwaka 2023 kikao kilichofanyika katika hotel ya aden palace Jijini mwanza
hivi karibuni
Wajumbe wa Bodi ya Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania ya Udhamini wa taarifa ya Juzuu la sheria Tanzania wakiwa katika picha ya Pamoja wakiongozwa na Mwenyekiti wa bodi hiyo ambaye pia ni Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania Mhe. Jacobs Mwambegele (aliyeketi katikakati) na kushoto kwake ni Profesa Hamudi Ismail Majamba wakiwa Pamoja na wa wajumbe wengine wanaounda bodi hiyo walipotembelea jengo la Mahakama la kituo Jumuishi cha Utoaji Haki jijini Mwanza iliyokutana hivi karibuni Jijini mwanza kwa ajili ya kujadili na kuandaa Juzuu ya taarifa ya sheria Tanzania ya mwaka 2023
Katibu wa Bodi ya
Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania ya Udhamini wa taarifa ya Juzuu la sheria
Tanzania Profesa Hamud Ismail Majamba akielezea jambo kwa wajumbe wa bodi hiyo (hawapo
pichani) wakati wa majadiliano juu ya uandaaji wa Juzuu ya sheria za Tanzania
kwa mwaka 2023 kikao kilichofanyika katika hotel ya aden palace Jijini mwanza
hivi karibuni.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni