Jumamosi, 9 Desemba 2023

MENEJIMENTI MAHAKAMA PWANI YAKUTANA

Menejimenti yamuaga pia Mhe. Devota Kisoka kufuatia kustaafu kwake

Na Eunice Lugiana, Mahakama-Pwani

Mahakama ya Hakimu  Mkazi  Pwani imefanya kikao cha Menejimenti, huku Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Mhe. Joyce Mkhoi akiwataka Mahakimu Wakazi mkoani humo kuwekeza muda wao katika kuujua mfumo mpya wa kuendesha mashauri (e-CMS). 

Akizungumza jana 08 Desemba, 2023 kikao hicho kilichofanyika  katika ukumbi wa Ofisi ya Taifa ya Mashitaka mkoani humo, Mhe. Mkhoi alisema kuwa, japo Mfumo bado ni mpya inawapasa Mahakimu wote kuufahamu maana ndio Mfumo unaotumika kwa sasa kusikiliza mashauri ambayo ndio kazi ya msingi ya Mhimili huo.

“Kwa kuwa kazi ya msingi ya Mahakama ni kusikiliza mashauri hivyo hakuna budi kila Hakimu kuufahamu Mfumo huu na kuufanyia kazi. Kama kuna mtu kwa namna yoyote ile anakwama katika usikilizaji wa mashauri ni vyema kuitumia siku hii kusaidiana na kuwekana sawa,” alisema Mhe. Mkhoi.

Katika kikao hicho, Mahakimu hao walishirikishana changamoto wanazokutana nazo kupitia Mfumo huo na kuzitatua kwa pamoja na kukubaliana kila changamoto na uvumbuzi wowote washirikishana ili kuendelea na kazi.

Akisoma taarifa ya Mahakama ya Wilaya Bagamoyo, Afisa utumishi wa Mahakama hiyo, Bw. Isihaka Mgude alisema katika kipindi cha mwezi Julai hadi Septemba mwaka huu Mahakama hiyo imefanikiwa  kukusanya   maduhuli ya zaidi ya Shilingi za Kitanzania milioni 50 kwa muda miezi mitatu.

Sambamba na kikao hicho, Menejimenti imefanya pia hafla fupi ya kumuaga aliyekua Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Kisarawe, Mhe. Devotha Kisoka aliyestaafu utumishi wa umma kwa mujibu wa Sheria.

Akitoa salaam za pongezi kwa mstaafu huyo,  Hakimu Mkazi Mfawidhi alisema, Mhe. Kisoka ameishi kwa kipindi chote cha utumishi wake kwa upendo  pia amemsifia kwa uharaka katika utendaji kazi wake.

“Kustaafu sio kuzeeka ziko shughuli zingine za kukufanya usichoke” alisema Mhe. Mkhoi .

Akitoa shukrani zake, Mhe. Kisoka alisema amefanya kazi na Mahakama kwa muda wa miaka 40 kuanzia akiwa binti mdogo mpaka sasa amestaafu.

“Nimeitumikia Mahakama kwa miaka 40 toka nikiwa binti mdogo na sasa nimestaafu niwatakie utumishi mwema watumishi wote mlioko kazini,” alieleza Mhe. Kisoka.

Katika hafla hiyo, zoezi la kukata keki aliyoandaliwa Mhe. Kisoka ilifanyanyika ambapo aliikata na kuwalisha watumishi wa Mahakama hiyo kama ishata ya upendo na kusema kwamba, Pwani ni mahali salama pa kufanya kazi kuna upendo na amani. 

Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Pwani,  Mhe. Joyce Mkhoi  akitoa neno wakati wa ufunguzi wa kikao cha Menejimenti ya Mahakama hiyo jana tarehe 08 Desemba, 2023 katika ukumbi wa Ofisi ya Taifa ya Mashitaka mkoani humo.

 Wajumbe wa Kikao cha Menejimenti ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Pwani wakifuatilia kinachojiri.

Afisa Utumishi Mahakama ya Wilaya Bagamoyo, Bw. Isihaka Mgude akiwasilisha taarifa ya Mahakama hiyo katika Kikao hicho.


Aliyekuwa Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya Kisarawe, Mhe. Devotha Kisoka akikata keki ya upendo aliyoandaliwa na Menejimenti ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Pwani kufuatia kustaafu kazi kwa mujibu wa sheria.

Mhe. Kisoka akimlisha keki Mtendaji wa Mahakama ya Mkoa wa Pwani, Bw. Moses Minga.

Mhe. Mkhoi (aliyesimama) akitoa nasaha na  pongezi kwa Mhe. Devotha Kisoka aliyestaafu Utumishi wa Umma.


 Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama Ya Wilaya Bagamoyo, Mhe. Samira Suleiman akikabidhi zawadi  ya picha kwa Mhe. Kisoka kwa niaba ya Menejimenti.

Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama Ya Wilaya Kisarawe, Mhe. Emmy Nsangalufu akimkabidhi zawadi Mtangulizi wake Mhe. Kisoka aliyestaafu utumishi wa umma.

Mhe. Herieth Mwailolo akikabidhi zawadi kwa Mhe. Kisoka.


Keki ya pongezi iliyoandaliwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Pwani kwa ajili ya kumpongeza Mhe. Kisoka kwa kustaafu salama utumishi wa umma.

(Habari hii imehaririwa na Mary Gwera, Mahakama-Dodoma)



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni