Na. Hilary Lorry – Mahakama, Lindi
Mkandarasi kutoka kampuni ya Uhandisi ya Kiure Limited
Bi. Irene Lugenge amekabidhiwa
eneo kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Mradi wa Mahakama ya Wilaya ya Nachingwea iliyopo
katika halmashauri ya Nachingwea wilaya ya Nachingwea Mkoa wa Lindi.
Mhandisi Mshauri kutoka kampuni ya OGM Consultant
Bw. Emmanuel Fovo
alieleza Ujenzi wa mradi wa Mahakama ya Wilaya ya Nachingwea ni wa miezi tisa
(9) na unatarajiwa kuanza rasmi tarehe 20 Disemba 2023 na kukamilika 20 Agosti 2024
kama mkataba unavyoeleza.
Bw.
Fovo alimtaka mkandarasi kuzingatia vipengele
vyote vilivyopo kwenye mkataba ili kuepuka changamoto zisizo za lazima na
kumshauri endapo atakutana na changamoto ni vyema akafanya mawasiliano na pande
zote zinahusika na mradi huu ili
isitokee tofauti yoyote na kuepuka ucheleweshwaji wa kukamilika kwa mradi.
Naye, Mhandisi wa Mahakama ya Tanzania Bw. Kelvin Juvinal alimtaka
mkandarasi kuzingatia sheria zote za usalama wakati wote wa ujenzi wa mradi na
kumtaka kuwa na vifaa vya huduma ya kwanza kwenye eneo la mradi. Vilevile
aliwataka mkandarasi na Mhandisi Mshauri kufanya kazi kama timu moja ili
kuhakikisha jengo linakamilika kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti Mtendaji wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi Bi.Quip Mbeyela na Hakimu mkazi
Mfawidhi Mahakama ya Wilaya ya Nachingwea Mhe.Sikitu Mwalusamba waliahidi kutoa ushirikiano wa karibu na
kufanya mawasiliano na pande zote zinahusika na ujenzi huo kwa lengo la
kuhakikisha ujenzi wa mradi huo unakamilika bila mkwamo wowote.
Aidha watumishi wa Mahakama ya Wilaya ya Nachingwea wamefurahia
sana kupokea mradi huo wa ujenzi kwani utawaondolea adha ya kutumia majengo ya
zamani na yenye miundo mbinu chakavu ambayo hayaendani na kasi ya sasa ya
Mahakama ya kuhamia katika matumizi ya Teknologia ya Habari na mawasiliano (TEHAMA).
Makabidhiano hayo yameshuhudiwa na mhandisi Emmanuel Fovo, Mhandisi Kelvin L.Juvinal na wenzake wawili kutoka Mahakama ya
Tanzania Makao Makuu, Mtendaji wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi Bi.Quip Godfrey Mbyela, pamoja na
Hakimu Mkazi mwandamizi Mahakama ya Wilaya ya Nachingwea Mhe. Sikitu Mwalusamba.
Makabidhiano ya mkataba kwaajili ya ujenzi wa Mahakama ya Wilaya ya Nachingwea kati ya mkandarasi kutoka kampuni ya Uhandisi ya Kiure BI. Irene Lugege (wa pili kushoto) na Mtendaji wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi Bi. Quip Mbeyela.(wa pili kulia)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni