Na. Paul Pascal – Mahakama, Moshi
Mtendaji
wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya moshi Bi. Maria Itala amefanya ukaguzi
katika jengo linaloendelea kufanyiwa kukarabati la Mahakama ya Mwanzo Kilema.
Ukaguzi
huo umefanyika tarehe 30 novemba 2023 ukiwa na lengo la kujionea maendeleo ya
uboreshaji wa miundo mbinu ya Mahakama hiyo ili kuweka mazingira rafiki ya utoaji
huduma kwa watumishi wa Mahakama pamoja na wananchi wa kata ya kilema kusini na
vitongoji vya jirani vilivyopo katika Wilaya ya Moshi Vijijini.
“Nipende
kuwahaikishia wananchi wote wa kilema kati na vijiji vya jirani ya kuwa mahkama
ya Tanzania itahakikisha jengo hili linakua bora na zuri kwa matumizi yetu sote
ili kuwezesha wananchi wote wanapata sehemu nzuri ya kupatia haki zao”, alisema
Mtendaji huyo
Ukarabati
wa Mahakama ya Mwanzo Kilema ulianza mwezi Oktoba 2023 na unatazamiwa
kukamilika tarehe 15 Desemba 2023 ukitekelezwa kwa fedha za ndani kutoka ofisi
ya Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Moshi ukiwa na thamani ya milioni 17, kukamilika
kwa ukarabati huu kutawezesha shughuli za kimahakama kufanyika katika jengo
linalomilikiwa na Mahakama ya Tanzania. Kwa sasa shughuli za Mahakama ya Mwanzo
Kilema zinaendeshwa katika jengo la serikali ya Kata ya Kilema Kusini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni