Na. Paul Pascal – Mahakama, Moshi
Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA) ambaye pia ni Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Barke Sehel amekutana na kushauriana na wanachama wa chama hicho mkoa wa Kilimanjaro.
Akizungumza katika mkutano ulifanyika ukumbi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi jana tarehe 12 Desemba, 2023 Mhe. Sehel alikutana na wananchama wa mkoa huo kwa mara ya kwanza toka aingie madarakani mwezi januari 2023.
“Nipende kuwashukuru kwa upendo mlionionyesha sina cha kuwalipa zaidi yakusema nitashirikiana nanyi siku zote vilevile niwashauri jambo moja tu ambalo ni tufanye kazi zetu kwa uadilifu, weledi na kujiamini, tukiweza kutimiza hilo hakika tutafika mbali katika taaaluma yetu”, alisema Mhe. Sehel
“Sisi kama TAWJA tunapaswa kuhakikisha tunatoa elimu katika hadhara zote za watanzania kila tunapopata nafasi yakufanya hivyo, kama kanda mnapaswa kuwa na mpango kazi (work plan) ili kuwezesha kufanikisha majukumu yenu ambayo kimsingi ni mwongozo wa chama chetu”, alisema Mhe. Sehel.
Mhe. Sehel
alibainisha mafanikio ambayo TAWJA wameyafikia tokea alipoingia ofisi Januari
2023 moja ya mafanikio hayo ni kufanikisha utoaji elimu kwa wiki ya sheria
iliyoanza mara tu baada ya uteuzi, kuhamasisha na kufanikisha ufadhili wa
wajumbe 10 kuhudhuria mkutano wa Morocco na wengine 21 walipata ufadhili wa
Mahakama, kuadhimisha siku ya Majaji wanawake Duniani inayofanyika kila mwaka
tarehe 10 mwezi wa Tatu.
Pamoja na mafanikio hayo Mhe. Sehel aliwataka wanachama hao kushiriki katika safari ya Ghana inayotarajiwa kufanyika mwezi Mei 2024, amesisitiza kulipa ada za uanachama kwasababu pamoja na mafanikio yote bado chama kina changamoto ya fedha za kujiendesha.
Akiongea katika mkutano huo mlezi wa TAWJA Kanda
ya Moshi Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Moshi Mhe. Dkt. Lilian
Mongela alimshukuru Mwenyekiti wa TAWJA Taifa kwa kuwapa nafasi hiyo adhimu ya kusalimiana
na kuongea machache, nikiwa kama mlezi nikuahidi na nikuhakikishishie pasi na
shaka Moshi unalo jeshi madhubuti hivyo basi yote uliyotuelekeza na kutushauri
tunakwenda kuvitekeleza kwa ufanisi wa hali ya juu.
Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA) ambaye pia ni Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Barke Sehel akiwa kwenye picha ya pamoja na wanachama wa chama hicho, kushoto ni Mlezi wa chama hicho Mkoani Kilimanjaro na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Moshi, Mhe. Lilian Mongella
Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA) ambaye pia ni Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Barke Sehel akifurahia jambo na Mlezi wa chama hicho Mkoani Kilimanjaro na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Moshi, Mhe. Lilian Mongella
Habari Hii Imehaririwa na Innocent Kansha - Mahakama
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni