Marehemu Godfrey Augustino Mpogole enzi za uhai wake.
TANZIA
Mahakama ya Tanzania inasikitika kutangaza kifo cha Mtumishi wake, Bw. Godfrey Augustino Mpogole aliyekuwa akihudumu Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Iringa kama Mtunza Kumbukumbu (RMA).
Kwa mujibu wa Kaimu Mtendaji Mahakama Kuu Kanda ya Iringa, Bi. Dorice Kisanga, marehemu Godfrey alikutwa na umauti ghafla jana tarehe 30 Desemba, 2023.
Amesema kuwa, mazishi yamefanyika leo tarehe 31 Desemba, 2023 katika Kijiji cha Kikombwe kilichopo mkoani Iringa.
Mahakama ya Tanzania inaungana na ndugu, jamaa na marafiki kuomboleza msiba huu wa kuondokewa na mpendwa wetu.
Bwana Alitoa na Bwana Ametwaa, Jina lake lihimidiwe.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni