CHALAMILA AWAALIKA WANANCHI KUPATA ELIMU YA UTATUZI WA MASUALA YA KISHERIA
Na Magreth Kinabo -Mahakama
Mkuu wa Mkao wa Dar es Salaam,Mhe. Albert Chalamila amesema Mahakama ndicho chombo kilichopewa dhamana ya kutafsiri sheria na kutoa haki bila kuiingiliwa na mtu yoyote, hivyo ni vema wananchi wakatumia nafasi hiyo ya wiki ya sheria kupata elimu ya masuala mbalimbali, ikiwemo migogoro ya ardhi na familia.
Hayo yamesemwa leo tarehe 27 Januari,2024 na Mkuu huyo wakati akizindua Wiki ya Sheria kwa upande wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam uliofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jiji Dar es Salaam, uliotanguliwa na matembezi kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu hadi kiwanjani hapo, ambapo alisema amekuwa migogoro hiyo ofisini kwake.
“Mahakama ndicho chombo muhimu cha kutafuta haki , ningependa kuwaomba wananchi wa Dar es Salaam watumie nafasi hiyo ya wiki ya Sheria kupata elimu juu ya masuala mbalimbali na kama wana shauri lililoko mahakamani bado waendelee kuona chombo kinachotoa haki hivyo wafike kiwanjani hapo kupata msaada wa kisheria,” alisema Mhe. Chalamila.
Akizungumzia kuhusu kauli mbiu ya Wiki na Siku ya Sheria ni ‘Umuhimu wa dhana ya haki kwa ustawi wa Taifa nafasi ya Mahakama na wadau katika kuboresha Mfumo Jumuishi wa Haki Jinai’ alisema inaendana na maboresho yanayoendelea kufanywa na Mahakama na Serikali kupitia Mfumo wa Haki Jinai, hivyo inajenga ushirikiano na wadau.
Alisema kauli mbiu hiyo inatekelezeka na kupimika juu ya mapendekezo yaliyomulikwa na Tume ya Haki Jinai.
Mhe. Chalamila alisema hata yeye kama kiongozi ana nafasi ya kupunguza mashauri mahakamani kwa kusimamia matendo mazuri yanayoleta imani.
Alimpongeza Rais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kuteua idadi kubwa ya Majaji wa Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu ya Tanzania.
Alimpongeza Jaji Mkuu wa Tanzania,Prof. Ibrahim Hamis Juma kutokana na maboresho yaliyofanywa na Mahakama hususan kwenye Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA).
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mhe. Albert Chalamila akitoa hotuba yake katika uzinduzi huo.
Baadhi ya watumishi wa kanda hiyo na wadau wakiwa katika matembezi hayo.
Picha namba 8995 ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam,Mhe. Salma Maghimbi akitoa hotuba yake.
Picha ya chini na juu ni Baadhi ya watumishi wa kanda hiyo na wadau wakiwa katika uzinduzi huo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni