Jumamosi, 27 Januari 2024

JITIHADA ZA RAIS SAMIA KUTETEA, KULINDA HAKI NCHINI NI DHAHIRI

Na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dodoma

Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanya jitihada kubwa katika kutetea na kulinda haki na imethibitisha kwa vitendo nia yake ya kuhakikisha kuwa mfumo wa haki nchini unaboreshwa.

Hayo yamebainishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma katika hafla ya uzinduzi rasmi wa Wiki ya Sheria katika Viwanja vya Nyerere Square leo tarehe 27 Januari, 2024, ambapo Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, Mhe. Dkt. Tulia Ackson alikuwa Mgeni Rasmi.

Jaji Mkuu ameeleza kuwa mara kadhaa Mhe. Dkt. Samia ametoa wito wa kuongeza kasi ya upelelezi wa mashauri ya jinai ili kulinda haki za watuhumiwa na amesisitiza kufanyika kwa maboresho katika mfumo wa haki jinai ili kutatua changamoto zilizopo. 

“Serikali inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan imethibitisha kwa vitendo nia yake ya kuhakikisha kuwa mfumo wa haki nchini unaboreshwa kwa kuunda Tume ya Haki Jinai kwa lengo la kupata changamoto za mfumo huo na kutoa mapendekezo,” amesema. 

Mhe. Prof. Juma amebainisha pia kuwa ili kuenzi jitihada zinazofanywa na Serikali, Mahakama imeamua mwaka huu 2024, kukaa pamoja na wadau wa haki jinai kujadiliana nafasi ya kila mmoja katika kuboresha mfumo wa utoaji haki nchini. 

“Pia tunalenga kutumia maadhimisho haya (Wiki ya Sheria) kutoa mrejesho kwa umma kuhusu ni kwa namna gani Mahakama imetekeleza maazimio ya Tume ya Haki Jinai... 

“Katika maonesho haya tumeweka banda moja maalum linalojumuisha wadau wote wa haki jinai ambao kila mmoja wetu atatumia fursa hii kutoa mrejesho kwa umma ni kwa namna gani Taasisi yake imetekeleza mapendekezo ya Tume ya Haki Jinai,” amesema. 

Hivyo, anawaalika wanachi wote kutumia fursa hiyo adhimu kupata mrejesho wa utekelezaji wa mapendekezo ya Tume ya Haki Jinai kutoka kwa wadau wote muhimu kwenye banda moja, jambo ambalo halitakuwa rahisi baada ya kipindi hiki.

Jaji Mkuu ameeleza pia kuwa kwenye Nchi ya demokrasia huwezi kuzungumuzia wadau wa haki bila kukitaja chombo chenye mamlaka ya kutunga sheria, yaani Bunge, ambalo ni mlinzi wa haki na hutekeleza hilo kwa kutunga sheria ambazo zinalinda haki za binadamu zilizotamkwa na Katiba pamoja na matamko mbalimbali ya Kimataifa juu ya haki za Binadamu. 

“Natambua kuwa zipo baadhi ya Sheria au vifungu ambavyo Tume ya Haki Jinai ilishauri vifanyiwe marekebisho ili kuboresha mfumo wa haki jinai. Ni matumaini yetu kuwa kufanyika kwa marekebisho ya sheria hizi pamoja na nyingine ambazo zinasababisha changamoto katika mchakato wa haki jinai kutaleta faida ya ustawi wa Tanzania,” amesema.

Mhe. Prof. Juma amesema kauli mbiu ya maadhimihso ya Wiki na Siku ya Sheria mwaka huu 2024 inasema, “Umuhimu wa Dhana ya Haki kwa Ustawi wa Taifa: Nafasi ya Mahakama na Wadau Katika Kuboresha Mfumo Jumuishi wa Haki Jinai."

Ameeleza kuwa kauli mbiu hiyo ni sehemu ya usemi kwamba hakuna nchi inayoweza kujitambulisha kuwa ni ya kidemokrasia na utawala bora kama haifuati misingi ya haki, kwani haki ni msingi wa uhuru, udugu, amani na utulivu ambao utatoa nafasi kwa shughuli za kisiasa, kiuchumi na kijamii kufanyika.

Kilele cha Maonesho ya Wiki ya Sheria kitafanyika tarehe 1 Februari, 2024 katika Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.


Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (juu na chini) akizungumza katika hafla ya uzinduzi rasmi wa Wiki ya Sheria katika Viwanja vya Nyerere Square leo tarehe 27 Januari, 2024.




Meza Kuu ikiongozwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, Mhe. Dkt. Tulia Ackson(katikati) katika picha ya pamoja kwenye uzinduzi wa Wiki ya Sheria Dodoma.

Meza Kuu ikiongozwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, Mhe. Dkt. Tulia Ackson(katikati) ikiwa katika picha ya pamoja na Majaji wa Mahakama ya Rufani.

Meza Kuu ikiongozwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, Mhe. Dkt. Tulia Ackson(katikati) ikiwa katika picha ya pamoja na Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Meza Kuu ikiongozwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, Mhe. Dkt. Tulia Ackson(katikati) ikiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Taasisi mbalimbali.

Meza Kuu ikiongozwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, Mhe. Dkt. Tulia Ackson(katikati) ikiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Tume ya Utumishi wa Mahakama.

Meza Kuu ikiongozwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, Mhe. Dkt. Tulia Ackson(katikati) ikiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Dodoma.

Meza Kuu ikiongozwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, Mhe. Dkt. Tulia Ackson(katikati) ikiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Menejimenti ya Mahakama ya Tanzania.

Meza Kuu ikiongozwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, Mhe. Dkt. Tulia Ackson(katikati) ikiwa katika picha ya pamoja na wanachama wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA).

Meza Kuu ikiongozwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, Mhe. Dkt. Tulia Ackson(katikati) ikiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Maandalizi.

Meza Kuu ikiongozwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, Mhe. Dkt. Tulia Ackson(katikati) ikiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa mabanda yanayoshiriki kwenye maonesho ya Wiki ya Sheria Dodoma.

Meza Kuu ikiongozwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, Mhe. Dkt. Tulia Ackson(katikati) ikiwa katika picha ya pamoja na vijana wanaofanya mazoezi kwa kukimbia, "jogging".



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni