Jumamosi, 27 Januari 2024

ELIMISHENI JAMII JUU YA TARATIBU ZA KIMAHAKAMA.

 

Richard Matasha -Mahakama  Mtwara

 

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mtwara, Mhe. Rose Ebrahim amewataka  watumishi wa Mahakama wa kanda hiyo, kutumia nafasi ya wiki ya sheria kuelimisha jamii juu ya taratibu za kimahakama.

 

Mhe, Ebrahim   alitoa rai hiyo leo tarehe 27 Januari,2024 kwenye uzinduzi wa wiki ya sheria nchini katika mkoa wa Mtwara ukiambatana na matembezi.

 

 Katika matembezi hayo yalijumuisha wadau mbalimbali wa Mahakama wakiwemo Ofisi ya Taifa ya Mwendesha Mashitaka(NPS), Jeshi la Polisi, Chama cha Wanasheria Tanganyika(TLS), Kampuni ya Mawasiliano ya Simu (TTCL) na benki mbalimbali na wengineo wengi wakiwa wameshika mabango yenye jumbe mbalimbali .

 

Mhe. Ebrahim akipokea halaiki hiyo ya matembezi aliwashukuru wadau hao kwa kuitikia wito wa    kushiriki  katika uzinduzi huo.

 

Jaji Mfawidhi, aliambatana na viongozi wa Mahakama Kuu kanda ya Mtwara ambao ni Majaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara Mhe. Martha Mpaze na Mhe Saidi Ding’ohi, Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara, Mhe Seraphine Nsana, Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara Bw. Richard Mbambe, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mtwara Mhe Charles Mnzava pamoja na watumishi wengine.

 

Matembezi ya uzinduzi  wa wiki ya sheria  yalichukua umbali wa takribani kilomita tano (KM 5) kutoka yalipoanzia katika viwanja vya Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara na kuhitimishwa katika viwanja vya Mahakama ya Mwanzo Mtwara Mjini. Vikundi mbalimbali vilishiriki katika matembezi hayo huku wakiwasilisha jumbe zao kwa mtindo wa mabango.

 

Katika Wiki ya Sheria mkoani Mtwara kumekuwepo na utoaji wa elimu kwa wananchi, huduma za upimaji wa afya, uchangiaji damu na matendo ya huruma kwa wahitaji. Shughuli hizo zimeleta msisimko mkubwa kwa wananchi na kuhamasika kutenga muda wao na kuja mabandani kupata huduma hizo.

 Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu  ya Tanzania Kanda ya Mtwara, Mhe. Rose . Ebrahim wa (katikati), Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara Mhe Martha Mpaze wa (kulia), na Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara, Mhe Saidi Ding’ohi(kushoto).


 Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Tanzania Kanda ya Mtwara, Mhe. Rose  Ebrahim wa () (aliyevalia kofia nyeupe), Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara Mhe Martha Mpaze wa (kulia), Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara, Mhe Saidi Ding’ohi wa (pili kushoto) na  Mtendaji wa Mahakama Kuu Mtwara Bw. Richard Mbambe wakiwa katika matembezi siku ya uzinduzi wa wiki ya sheria nchini mwaka 2024.

 

 Watumishi na wadau wa mahakama wakiwa wanafwatilia matukio kwa bashasha katika viwanja vya Mahakama ya Mwanzo Mtwara Mjini wakati wa uzinduzi wa wiki ya sheria nchini mkoani Mtwara mwaka 2024.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara, Mhe. Rose  Ebrahim akisikiliza jambo pindi alipozuru moja ya banda la maonesho na utoaji elimu katika viwanja vya Mahakama ya Mwanzo Mtwara mjini wakati wa uzinduzi wa wiki ya sheria nchini mkoani Mtwara mwaka 2024.

Jeshi la polisi dawati la jinsia wakiwa wameshiriki  katika matembezi ya ufunguzi wa wiki ya sheria nchini mkoani Mtwara .

 

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni