Na. Hilary Lorry – Mahakama, Lindi
- Wafurahishwa
na jitihada za Mahakama kuwafikia walipo.
- Wavutiwa na mada mbalimbali zinazowasilishwa na watoa elimu waliobobea katika masuala mbalimbali ya kisheria.
- Waipongeza mahakama kwa uwazi na huduma bora wanazozitoa.
- Waipongeza Mahakama kwa ushirikiano mzuri na wadau.
Viongozi wa Mahakama Mkoa wa Lindi wakiongozwa na
Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Hakimu mkazi Lindi Mhe. Consolata Singano kwa
nyakati tofauti walitoa wito kwa wananchi Mkoa wa Lindi kujitokeza kwa wingi kwenye
maadhimisho ya wiki ya sheria nchini ili kupata elimu na kujifunza mambo
mbalimbali yanayofanywa na Mahakama katika mchakato mzima wa upatikanaji wa
haki.
Wiki ya elimu inachagizwa na kauli mbiu isemayo “Umuhimu Wa Dhana Ya Haki Kwa Ustawi Wa
Taifa: Nafasi Ya Mahakama Na Wadau Katika Kuboresha Mfumo Jumuishi Wa Haki
Jinai’’
Katika kuitikia wito Wananchi mkoani Lindi wameendelea
kujitokeza kwa wingi katika mabanda ya
maonyesho ya wiki ya sheria yaliyopo
mkabala na hotel ya sea view katika
viwanja vya mpira wa kikapu kupata msaada wa kisheria, elimu, kujua taratibu za
kimahakama na mambo mengine kemkem yanayowasilishwa na watumishi wa Mahakama
pamoja na wadau mbalimbali wanaoshiriki zoezi la utoaji elimu.
Aidha, wananchi wamefurahishwa na jitihada za Mahakama
kuwafikia wananchi popote walipo kwa kutembelea maeneo ya mikusanyiko, mashuleni,
vyuo, na kuwatenegenezea mazingira mazuri ya kupata elimu na vipindi mbalimbali
vya redio. Vilevile walitoa pongezi za dhati kwa uwasilishwaji wa mada
zinazogusa kila nyanja katika jamii zilizowasilishwa kwa kina na wabobezi
katika tasnia ya sheria.
Sambamba na hilo, wananchi mkoani Lindi wameipongeza Mahakama
ya Tanzania kwa uwazi na huduma bora wanayoendelea kuitoa kwa wananchi. Na pia wamefurahishwa
na ushirikishwaji mzuri wa wadau katika zoezi zima la utoaji elimu maredioni na
katika majukwaa mbalimbali.
Hakimu
Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya ya Lindi mhe.Maria Amos Batulaine wa kwanza
kulia akiambataana na waheshimiwa wengine wawili akiwa redio mashujaa kutoa
wito kwa wananchi mkoa wa Lindi kujitokeza kwa wingi katika mabanda ya utoaji elimu.
Msaidizi wa kumbukumbu Bi. Mwanakombo
Ally akitoa elimu juu ya hatua zinazotakiwa kufuatwa wakati wa ufunguaji wa
shauri kwa mmoja wa wateja aliyewasilisha hoja ya kutaka kujua hatua za ufunguaji wa shauri.
Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Mwanzo
Nga’pa Mhe. Patricia Mombo akiwasilisha mada kwa wanafunzi wa Chuo cha Uuguzi
Lindi Mjini.
Zoezi la kupanda miti ni moja kati ya
mambo yanayofanywa katika wiki hii ya sheria Mkoa wa Lindi.
Zoezi la kupanda miti ni moja kati ya
mambo yanayofanywa katika wiki hii ya sheria Mkoa wa Lindi.
Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya
Mwanzo Lindi Mjini Mhe.Illuminata Lutakana akitoa elimu kwa moja kati ya wateja
waliofika kupata huduma ya elimu katika banda la Mahakama.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni