Na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dodoma
Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Bw Aretas Lyimo ameipongeza Serikali kwa kuunganisha wadau wa haki jinai ili kuharakisha utoaji wa haki kwa wananchi.
Kamishna Jenerali ametoa pongezi hizo leo tarehe 29 Januari, 2024 wakati anatembelea mabanda ya maonesho ya Wiki ya Sheria yanayofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Nyerere Square jijini hapa.
Amesema kuwepo kwa umoja na ushirikiano kati ya wadau wa haki jinai kunarahisisha utendaji na kuleta matokeo chanya, hivyo akashauri Taasisi zinazohusika kuuendeleza na kufanya kazi kwa pamoja.
Kadhalika, Kamishna Jenerali aliwaomba wadau hao kuimarisha mahusiano na kuongeza utoaji wa elimu kwa wananchi ili kuongeza uelewa na kuwaondolea uoga kwani ushirikiano wao ni muhimu katika maeneo yao ya utendaji.
Baadhi ya mabanda aliyotembelea ni Mapokezi, Wadau wa Haki Jinai, Magereza, Uhamiaji,Taasisi ya Kuthibiti na Kupambana na Rushwa, Polisi, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Mkemia Mkuu wa Serikali na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, kama picha chini zinavyojieleza.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni