Jumatatu, 29 Januari 2024

MKUU WA WILAYA LINDI AWAALIKA WANANCHI KUJITOKEZA KUPATA ELIMU YA SHERIA

Na. Hilary Lorry-Mahakama, Lindi

Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi imeungana na Mahakama zingine nchini kuadhimisha siku ya uzinduzi rasmi wa wiki ya sheria uliofanyika tarehe 27 Januari, 2024. Zoezi la uzinduzi wa wiki ya Sheria lilianza kwa matembezi yaliyoongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe.Shaibu Ndemanga na viongozi wengine waandamizi wa Mahakama.

Akizungumza na mamia ya watu waliohudhuria matembezi hayo, Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe. Ndemanga aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupata elimu ya sheria inayotolewa bila malipo yeyote na Mahakama ya Tanzania.

Mhe. Ndemanga aliipongeza Mahakama ya Tanzania kwa mabadiliko makubwa waliyoyafanya hasa akigusia nguzo tatu za Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania wa 2020/2021-2024/2025, kwa kusema hakika Mahakama ya Tanzania inauishi Mpango Mkakati huo kwani miundombinu ya kisasa ipo kila mahali nchini na matumizi ya kielektroniki yanazidi kustawisha katika utoaji haki kwa wananchi hiyo ni hatua kubwa sana.

Naye, Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi Mhe. Consolata Peter Singano alimshukuru mgeni rasmi, wadau na wananchi wote kwakujitokeza kwa wingi katika uzinduzi rasmi wa wiki ya sheria Nchini.

Mhe. Singano pia aliwataka wananchi waendelea kujitokeza kwa wingi kupata elimu inayotelewa na Mahakama katika majukwaa mbalimbali kipindi hichi cha wiki ya sheria.

Katika kuadhimisha siku hiyo matembezi yalianza katika viunga vya Mahakama ya Mwanzo Lindi Mjini kuzungukia fisi kuelekea uwanja wa kikapu uliopo mkabala na Hoteli ya Sea view ambapo Umma ulioshiriki maandamano ulipata wasaa wakusikiliza hotuba kutoka kwa viongozi hao.

Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe. Shaibu Ndemanga aliyevaa kofia yenye nembo ya bendera ya taifa (katikati) akihutubia umati ulioshiriki maandamano ya uzinduzi wa wiki ya sheria.

Hakimu Mkazi Mfawidhi Mkoa wa Lindi. Mhe Consolata Peter Singano (aliyeshika karatasi mkononi) akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi na umati uliofika katika uzinduzi rasmi wa wiki ya sheria.

Meza Kuu ikiwa kwenye picha ya pamoja ya wadau na watumishi walioshiriki zoezi la uzinduzi wa wiki ya sheria

Meza Kuu ikiwa kwenye picha ya pamoja ya wadau na watumishi walioshiriki zoezi la uzinduzi wa wiki ya sheria

Mkuu wa Wilaya Lindi Mhe. Shaibu Ndemanga (wa pili kushoto) na Sehemu ya Watumishi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi, wadau na wananchi wakishiriki matembezi ya kuashiria uzinguzi wa wiki ya sheria nchini.

Sehemu ya Watumishi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi, wadau na wananchi wakishiriki matembezi ya kuashiria uzinguzi wa wiki ya sheria nchini.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni