Na.
Mwinga Mpoli – Mahakama, Mbeya
Majaji, Mahakimu, Watumishi na Wadau wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mbeya jana tarehe 24 Januari, 2024 waliungana kuhakikisha wanatoa elimu na msaada wa sheria kwa taasisi na makundi mbalimbali jijini Mbeya kuhakikisha wiki ya sheria inakuwa yenye mafanikio
Akiongea
na wakufunzi pamoja na wanafunzi wa Chuo cha Mzumbe tawi la Mbeya Jaji wa
Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mbeya Mhe. Victoria Nongwa alitoa mada ya
unyanyasaji wa kingono mitandaoni pamoja na makosa dhidi ya utu na aina
mbalimbali za makosa hayo.
“Unyanyasaji
wa Kingono hasa katika Mitandao umeshika kasi katika jamii pamoja na makosa
dhidi ya utu, na waathirika wakubwa ni wanafunzi, ni vizuri mitandao tuitumie
kupata elimu kuliko kuitumia tofauti, vinginevyo tutajikuta tukiingia kwenye
matatizo ya kukizana na sheria jambo ambalo linaweza kuharibu malengo ya mtu
binafsi na jamii inayotuzunguka” alisema Mhe. Jaji Nongwa
Naye,
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya Mhe. Emmanuel Kawishe
aliwakumbusha wanafunzi hao, sheria mbalimbali zinazoengelea makosa dhidi ya
utu na kwa jinsi gani makosa hayo yana athari kwa jamii.
Kwa
upande mwingi kwenye mdahalo huo Hakimu Mkazi Mhe. Hafsa Shelimo alieleza juu
ya Rushwa ya ngono inayofanywa na watu wenye mamlaka hasa mashuleni na vyuoni na
kuwatahadharisha wanafunzi hao kuwa kwa kushiriki matendo hayo bila kuyafichua
yanachangia kiasi kikubwa kuporomosha maadili na kutengeneza wataalum wasio
kuwa na ufanisi na weledi katika kutekeleza majukumu yao.
Naye,
Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Mwanzo Mbeya Mjini Mhe. Asha Njovu akitoa
elimu katika shule ya Sekondari Old Airport alitoa mada kwa Walimu na
Wafanyakazi wa Shule hiyo juu ya masuala ya Talaka na vitu vinavyosababisha
Mahakama kuvunja ndoa na mgao wa mali mara baada ya ndoa kuthibitika kuvunjika.
Kwa
upande wake Hakimu Mkazi Mhe. Abdulazizi Nchimbi alitoa elimu ya Mirathiv na
kuwakumbusha watumishi wa shule hiyo kuandika wosia ili kuepusha mali walizochuma
kupotea bila kuwanufaisha warithi halali.
“Kwani
uzoefu umekuwa ukionyesha kuwa kuna baadhi ya wasimamizi wa mirathi
wanaoteuliwa na Mahakama kutokuwa waaminifu na hufuja mali za maerehemu bila
kujali wanufaika wa mali hizo na kusababisha migogoro isiyokwisha kwa wakati na
kuathiri ustawi wa familia husika,” aliongeza Mhe. Nchimbi.
Naye,
Mdau kutoka Jeshi la Polisi Insp. Loveness Mtemi na Asp. Veronica Ponela ambaye
ni Mkuu wa Dawati la Jinsia Mkoa wa Mbeya waliwaeleza wanafunzi juu ya makosa
ya ukatili wa kijinsia, ubakaji na hata mimba za utotoni na hatua za kuchukua
mara tu dalili za kufanyiwa vitendo hivyo viovu zinapoonekana.
Wakitoa
elimu katika Shule ya Msingi Madaraka Hakimu Mkazi Mhe. Dickson Mmasi pamoja na
Wakili wa Serikali kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Bw. Rajabu Msemo waliwakumbusha
wanafunzi suala zima la makosa ya kijinsia na ukatili wa kingono kwa watoto
wadogo, makosa ya madawa ya kulevya na madhara yake kwa jamii na pia kuwataka
wanafunzi kusoma kwa bidii na kujiepusha na kukizana na sheria.
Jopo la watoa
elimu katika Chuo Kikuu cha Mzumbe tawi la Mbeya wakiongozwa na Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Mhe. Victoria Nongwa (wa pili
kushoto) wakiwa kwenye picha ya pamoja. Wengine ni Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Mzumbe tawi la Mbeya Prof. Henry
Mollel (wa tatu kushoto) na wa tano kutoka kulia ni Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mhe. Emmanuel Kawishe.
Sehemu ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe tawi la Mbeya wakifuatilia elimu inayotolewa kwa umakini
Sehemu ya Mahakimu na wadau kutoka Jeshi la polisi waliotembelea Shule ya Sekondari Old Airport kutoa elimu ya sheria.
Asp. Veronica
Ponela ambaye ni Mkuu wa Dawati la Jinsia Mkoa wa Mbeya akiwaeleza wanafunzi
jambo
Sehemu ya
wanafunzi wa Shule ya Sekondari Old Airport wakisikiliza kwa umakini elimu wanayopatiwa.
Hakimu Mkazi Mhe. Dickson Mmasi akitoa elimu ya sheria kwa wanafunzi wa shule ya msingi Madaraka.
Kushoto ni Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya Mbeya Mhe. Tedy Mlimba na kulia ni Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Mwanzo Santilya Mhe.
Mayonga Manyeresa wakielezea dha ya kauli mbiu ya wiki ya sheria na siku ya sheria nchini kupitia kituo cha redio Bigstar Fm 106.5 Mbeya
Sehemu ya watoa elimu ya sheria kutoka Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA).
Washiriki wa kutoa
elimu kutoka Taasisi Mbalimbali za Umma wakiwa tayari kutoa elimu na msaada wa kisheria katika viwanja vya kabwe jijini Mbeya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni