Na. Mwandishi Wetu, IJA
Jaji wa Mahakama ya Rufani na Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) Mhe. Dkt. Paul F. Kihwelo amefunga mafunzo ya maandalizi na matumizi ya jukwaa la kufundishia kwa njia ya mtandao ‘e-learning’ ambalo limeandaliwa na Mahakama ya Tanzania kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa watumishi wake kwa njia ya mtandao.
Mafunzo hayo yalifungwa Ijumaa tarehe 19 Januari, 2024 Chuoni Lushoto na yaliandaliwa na Mahakama ya Tanzania kwa kushirikiana na Chuo ambapo washiriki walikuwa ni Majaji, Manaibu Wasajili, Mahakimu Wakazi, Maafisa Utumishi/Tawala, Maafisa TEHAMA pamoja na Afisa habari.
Katika nasaha zake za kufunga mafunzo hayo, Mhe. Kihwelo amewaambia washiriki wa mafunzo hayo kuwa wana wajibu wa kuisaidia Mahakama ya Tanzania katika utekelezaji wa mfumo huo wa Mafunzo mtandao.
"Miye naamini mnaondoka hapa tofauti na mlivyokuja, hamuondoki bila kitu, pia tunaondoka tukiwa na wajibu mkubwa wa kusaidia Mahakama katika mfumo huu wa mafunzo mtandao," amesema Mhe. Kihwelo.
Pia Mhe. Kihwelo ameelezea kufurahishwa na wawezeshaji wa mafunzo hayo akisema kuwa wamefundisha kwa njia ambazo zimewafanya washiriki waweze kulielewa jukwaa hilo la kufundishia kwa njia ya mtandao kwa njia rahisi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa Mafunzo ya Mahakama Bi. Patricia Ngungulu amewapongeza washiriki wa mafunzo hayo na kuwanasihi wakayafanyie kazi yale waliyojifunza ikiwemo kuwafundisha watumishi wengine wa Mahakama.
Naye, mshiriki ambaye alitoa neno la shukrani kwa niaba ya wenzake Afisa Tawala Mahakama ya wilaya ya Kibiti Bw. Shadrack Mlomo amesifu mafunzo hayo na kuahidi kuwa wao washiriki wana wajibu wa kuhakikisha mfumo huo unafanya kazi kama ilivyokusudiwa.
Pia ameipongeza Mahakama ya Tanzania kwa kujenga jukwaa hilo kwa watumishi wa Mahakama na kwamba kuanzishwa kwake kunaleta maana halisi ya Mahakama mtandao.
Jukwaa hilo la kujifunzia mtandaoni
limetengenezwa na wataalamu wa ndani ya Tanzania ambao ni kutoka Mahakama ya
Tanzania, IJA, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na Chuo cha Serikali za Mitaa
(Hombolo), na ni utekelezaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Kuelekea Tanzania ya
Kidigiti (Digital Economy Strategic Framework (2023-2033) pamoja na National
ICT Policy 2023 ambavyo kwa pamoja vinachagizwa na Mradi wa Kidigiti wa Taifa
(Digital Tanzania Project-DTP).
Jaji wa Mahakama ya Rufani na Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) Mhe. Dkt. Paul F. Kihwelo (aliyekaa katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Washiriki wa Mafunzo ya maandalizi na matumizi ya jukwaa la kufundishia kwa njia ya mtandao ‘e-learning’ ambao ni Majaji, Manaibu Wasajili, Mahakimu Wakazi, Maafisa Utumishi/Tawala, Maafisa TEHAMA pamoja na Afisa Habari. Wengine meza kuu ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya Mhe. Victoria Nongwa(kushoto) pamoja na Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya ya Lushoto Mhe. Rose Ngoka (kulia) wakati wa kufunga mafunzo hayo.
Jaji wa Mahakama ya Rufani na Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) Mhe. Dkt. Paul F. Kihwelo akihutubia wakati wa kufunga mafunzo ya maandalizi na matumizi ya jukwaa la kufundishia kwa njia ya mtandao ‘e-learning’ ambalo limeandaliwa na Mahakama ya Tanzania kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa watumishi wake kwa njia ya mtandao. Mafunzo hayo yalifunguwa tarehe 19 Januari, 2024 Chuoni Lushoto na yaliandaliwa na Mahakama ya Tanzania kwa kushirikiana na Chuo ambapo washiriki ni Majaji, Manaibu Wasajili, Mahakimu Wakazi, Maafisa Utumishi/Tawala, Maafisa TEHAMA pamoja na Afisa Habari.
Sehemu ya Washiriki wa Mafunzo ya maandalizi na matumizi ya
jukwaa la kufundishia kwa njia ya mtandao ‘e-learning’ wakifuatilia hotuba ya
mgeni rasmi Mhe. Dkt. Paul F. Kihwelo (hayupo pichani) wakati akifunga mafunzo
hayo.
Sehemu ya Washiriki wa Mafunzo ya maandalizi na matumizi ya jukwaa la kufundishia kwa njia ya mtandao ‘e-learning’ wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Mhe. Dkt. Paul F. Kihwelo (aliyesimama kwenye podiamu) wakati akifunga mafunzo hayo.
Jaji wa Mahakama ya Rufani na Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa
Mahakama Lushoto (IJA) Mhe. Dkt. Paul F. Kihwelo akimpatia zawadi ya Chuo Mkurugenzi
Msaidizi wa Mafunzo Mahakama ya Tanzania Bi. Patricia Ngungulu wakati wa
kufunga mafunzo ya maandalizi na matumizi ya
jukwaa la kufundishia kwa njia ya mtandao ‘e-learning’ ambalo limeandaliwa na
Mahakama ya Tanzania kwa ajili ya kutoa mafunzo
kwa watumishi wake kwa njia ya mtandao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni