Na. Stephen Kapiga -Mahakama Mwanza.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza Mhe. Dkt. Ntemi Kilekamajenga amefanya kikao cha pamoja na watumishi wote wa Mahakama zilizopo kanda ya Mwanza kwa lengo la kuona namna bora ya kuwezesha watumishi wote wa Kanda hiyo wanashiriki utoaji elimu kwa wiki hiyo na hatimaye kilele cha siku ya sheria nchini Mosi Februari, 2024
Akizungumza katika hicho Mhe. Dkt. Kilekamajenga aliwahimiza Mahakimu wa Mahakama za mwanzo zilizopo kanda hiyo kuhakikisha kuwa wanashiriki kikamilifu katika wiki ya sheria nchini na pia ratiba zao za mashauri Mahakamani haziwazuii wao ama Wasaidizi wa Kumbukumbu wa Mahakama hizo kuweza kushiriki maadhimisho hayo.
Aidha,
Mhe. Dkt. Kilekamajenga aliainisha mpango uliofanywa kwa ajili ya kuwafikia
waendesha bodaboda wote waliopo jijini Mwanza kwa kushirikiana na viongozi wa
vyama vya waendesha bodaboda ili waweze kupewa elimu ya sheria katika Nyanja mbalimbali
ikiwa ni pamoja na elimu ya sheria ya mikataba, elimu ya sheria za barabarani,
elimu ya sheria ya usafirishaji wa abiria pamoja na elimu ya sheria ya bima ya
vyombo vya moto kwa lengo la kuwasidia waendesha bodaboda hao ambao wengi wao
wamekuwa wakikumbana na changamoto wakati wa kutekeleza majukumu yao.
Sehemu ya watumishi
wa Mahakama zilizopo kanda ya Mwanza wakifuatilia kwa makini maelekezo ya Jaji Mfawidhi
Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mwanza Mhe. Dkt. Ntemi Kilekamajenga (hayupo
pichani) alipokuwa akiongea nao juu ya maandalizi ya kuweza kufanikisha wiki na
siku ya sheria nchini inayotarajiwa kuanza tarehe 24 Januari, 2024 katika
viwanja vya Furahisha Jijini Mwanza.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni