Alhamisi, 25 Januari 2024

JAJI MAGHIMBI AHIMIZA WANANCHI KUJITOKEZA KUPATA ELIMU YA SHERIA

Na. Mwandishi Wetu.

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam Mhe. Salma Maghimbi jana tarehe 24 Januari, 2024 alizindua maonyesho ya wiki ya sheria yanayoambata na utoaji wa elimu na msaada wa kisheria kwa wananchi yanayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini hapo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo ulioambanata na kutembelea madanda ya maonyesho hayo ya Wiki ya Sheria kwa Mwaka 2024, Mhe. Maghimbi alisema maonyesho hayo yanahusisha utoaji wa elimu ya kisheria bure kwa wadau wa Mahakama yenye kauli mbiu isemayo “Umuhimu wa dhana ya haki kwa ustawi wa Taifa, nafasi ya Mahakama na wadau katika kuboresha mfumo jumuishi wa haki jinai”.


“Napenda kuchua fursa hii kuwakumbusha wananchi wote kutembele mabanda yetu ili kupata elimu ili kujenga uelewa wa mambo mbalimbali ya kisheria kwani hii ni nafasi adhimu inayotokea mara moja kila mwaka, tungependa kuona wananchi wengi wanafaidika kupitia zoezi hili la wiki ya sheria”, alisema Mhe. Maghimbi.


Vile vile Mhe. Maghimbi alisema, matembezi ya Uzinduzi wa Wiki ya Sheria mwaka 2024 yatafanyika tarehe 27 Januari, 2024. Matembezi yanatarajia kuanzia viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, muda wa saa 12 kamili asubuhi kuelekea viwanja vya Mnazi Mmoja ambapo maonyesho ya wiki ya sheria yanaendelea na wiki ya utoaji elimu itahitimishwa tarehe 30 Januari, 2024, na siku ya kilele cha Sheria itaadhimishwa tarehe 01 Februari, 2024 katika viwanja vya Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam. 

Awali maonyesho hayo yalitembelewa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Ardhi Mhe. Elineza Luvanda ambaye alitembelea mabanda ya wadau mbalimbali na kupata elimu na kubadilishana uzoefu katika masuala ya sheria

Maonyesho hayo yameanza jana tarehe 24 Januari, 2024 nchi nzima yakiwashirikisha wadau mbalimbali wa sheria. Mhe. Maghimbi aliambatana na Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam Mhe. David Ngunyale, Naibu Msajili Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam Mhe. Sundi Fimbo.

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam Mhe. Salma Maghimbi (mwenye ushungi) akikagua banda la Masjala Kuu litakalo tumika kutolea elimu kwa wananchi katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam jana tarehe 24 Januari, 2024 na pendeni yake ni Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam Mhe. David Ngunyale.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Ardhi Mhe. Elineza Luvanda akichukua kitabu cha wageni alipotembelea banda la Mahakama Kuu ya Tanzania Kituo cha Usuluhishi.


Sehemu ya wananchi waliofika kupata huduma katika Banda la Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi 

Sehemu ya wananchi waliofika kupata huduma katika Banda la Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini - RITA wakipata huduma 

Sehemu ya mwananchi aliyefika kupata huduma katika Banda la mfuko wa fidia kwa wafanyakazi
Sehemu ya mwananchi aliyefika kupata huduma katika Banda la Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania - TAWJA


Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam Mhe. Salma Maghimbi (mwenye ushungi) akibadilisha mawazo na viongozi mbalimbali waliofika  katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam jana tarehe 24 Januari, 2024 na pendeni yake kushoto ni Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam Mhe. David Ngunyale.

Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam Mhe. David Ngunyale akisaini Kitabu cha Wageni.


Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam Mhe. Salma Maghimbi (Katika) akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi 
Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam Mhe. Salma Maghimbi (Mwenye koti la bluu) akibadilishana mawazo na wananchi waliokuwa wanapata huduma kwenye banda la Mahakama za Wilaya za Mkoa wa Dar es salaam.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni