Jumanne, 30 Januari 2024

JAJI NDUGURU ATEMBELEA MAHABUSU YA WATOTO MBEYA

Na. Mwinga Mpoli – Mahakama Mbeya

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya Mhe. Dunstan Ndunguru ametembelea mahabusu ya watoto iliyopo mkoani humo jana tarehe 29 Januari, 2024 ikiwa na lengo la kutekeleza shughuli mbalimbali zinazoambatana na maadhimisho ya wiki ya sheria na kilele cha siku ya sheria nchini.

Mhe. Ndunguru amewaeleza watoto katika mahabusu hiyo namna ambavyo wanatakiwa kubadili mienendo yao na kutokinzana na sheria wawapo uraiani. Amewataka kuwa watulivu na wasione kama wametengwa ni katika hali ya kuwaweka sawa ili kesho wawe watu wema na wenye mafanikio.

“Hakika umri wenu bado ni mdogo hamtakiwi kujihusisha katika makosa ya namna yoyote na mnatakiwa kujiepusha na makundi yasiyofaa ambayo yanapelekea watoto kukinzana na sheria”

Aidha kwa upande wa kutoa elimu katika maadhimisho hayo ya wiki ya sheria Mhe. Martin Mwansasu ameongoza jopo lililokwenda shule ya sekondari Forest wakati Mhe. Upendo Moshi yeye akiongoza jopo la watu lililokwenda shule ya Msingi Mwasanga. Alikadhalika wananchi wameendelea kujitokeza kwa wingi kupata elimu kuhusu masuala mbalimbali ya kisheria katika maeneo mbalimbali ya jiji la mbeya.

Sanjali na Mhe. Dunstan Ndunguru aliambatana na Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Mhe. Victoria Nongwa, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Mbeya Mhe. Tedy Mlimba, waheshimiwa Mahakimu, wakili wa serikali, wakili wa kujitegemea na wadau wengine wa Mahakama. 

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Mhe. Dunstan Ndunguru wanne kushoto akiwa watumishi wa Mahakama pamoja na wadau alipotembelea Mahabusu ya watoto iliyopo jijini Mbeya. Na watatu kulia ni Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Mhe. Victoria Nongwa

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Mhe. Dunstan Ndunguru na Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Mhe. Victoria Nongwa wakiwa wameambatana na watumishi wa Mahakama pamoja na wadau mbalimbali wakimsikiliza Afisa Ustawi wa Jamii akitoa maelezo ya namna ya kurekebisha tabia za mahabusu watoto.

Watumishi wa Mahakama, Walimu na wadau wa Mahakama katika shule ya Sekondari Foresti.

Wanafunzi wa shule ya Sekondari Foresti wakimsikiliza elimu ya sheria iliyotolewa shuleni hapo ikiwa ni jitihada za kuzifikia taasisi mbalimbali wakati wa maadhimisho ya wiki ya sheria 

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mwasanga wakisikiliza elimu ya sheria.

 




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni