Jumanne, 30 Januari 2024

MAHAKAMA MBEYA YASHEREHESHA WIKI YA SHERIA KWA BONANZA

Na. Mwinga Mpoli – Mahakama Mbeya 

Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya imefanya bonanza jana tarehe 28 Januari, 2024 ikiwa ni kusherehesha shughuli za maadhimisho ya wiki ya sheria na siku ya Sheria nchini kwa lengo la kuhamasisha wananchi waweze kujitokeza kupata elimu ya sheria na kujielimisha kuhusu mambo mbalimbali mtambuka ya kimahakama.

Akizungumza wakati wa bonanza hilo mgeni rasmi Naibu Mstahiki Meya wa jiji la Mbeya Mhe. Kefasi Mwasote aliishukuru Mahakama kwa kuweza kufanya bonanza ilo kwani sio tu kupata elimu ila na kuhakikisha afya za watumishi na wadau zinakuwa imara.

“Ni furaha kutoa zawadi kwa washindi mbalimbali walioshinda michezo iliyohusisha bonanza la leo niuombe uongozi na waandaaji tusiishie kuandaa michezo hii wakati wa wiki ya sheria zoezi hili liwe endelevu kwani michezo ni afya na uleta mshikamano”, aliongeza Mhe. Naibu Mstaki Meya.

Naibu Mstahiki Meya wa jiji la Mbeya Mhe. Mwasote katika bonanza hilo aliungana na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Mhe. Dunstan Ndunguru, waheshimiwa Majaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, Manaibu wasajili, watumishi wa Mahakama, wadau wa Mahakama, wanafunzi pamoja ni vilabu vya marathoni vya mkoa wa Mbeya.

Bonanza lilifanyika katika viwanja vya Chuo cha Usimamizi wa Fedha Mbeya na kulifanyika michezo mbalimbali kama vile mpira wa miguu, mpira wa pete, kuvuta Kamba, kukimbiza kuku, kukimbiza sungura, kukimbia na magunia, kukimbia na mayai, mpira wa kikapu iliyohusisha watumishi wa Mahakama na wadau wengine.

Watumishi wa Mahakama wanawake wakishangilia ushindi baada ya kuibuka washindi katika mchezo wa kuvuta Kamba dhidi ya watumishi wa Mahakama Wakiume.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Mhe. Dunstun Ndunguru (aliyeshika kamba) akikabidhi zawadi ya Mbuzi kwa washindi.

Mgeni Rasmi Naibu Mstahiki Meya wa jiji la Mbeya Mhe. Kefasi Mwasote akifuatilia mchezo wa mpira wa miguu.

Watumishi wa Mahakama katika mchezo wa kuvuta kamba.

Watumishi wa Mahakama Mpira wa miguu wakimenyana katika mchezo wa Mpira wa miguu dhidi ya benk ya NMB

 





 


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni