Mahakama ya Hakimu Mkazi Simiyu imefanya bonanza leo tarehe 26 Januari, 2024 ikiwa moja ya maadhimisho ya Wiki ya Sheria na kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kupata elimu juu ya masuala mbali mbali ya kisheria.
Mgeni rasmi katika bonanza hilo alikuwa Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Simiyu, Mhe. Martha Mahumbuga ambaye aliambatana na Mtendaji wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Simiyu, Bw. Gasto Kanyairita na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Bariadi, Mhe. Caroline Kiliwa.
Watumishi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Simiyu, Mahakama ya Wilaya Bariadi na watumishi wa Gereza la Wilaya Bariadi walianza matembezi ya pamoja kutoka katika Viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Simiyu kuelekea katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Bariadi.
Bonanza lilichezwa katika viwanja hivyo na kuchezwa michezo mbalimbali ya kirafiki, ikiwemo mpira wa miguu, mpira wa pete, riadha na kuvuta kamba.
Mahakama iliibuka kidedea katika michezo yote, ambapo mpira wa pete ilipata goli 8: 4, mchezo wa kuvuta kamba akawaaragaza Magereza hali, huku kwenye riadha ikitimua vumbi na baadaye kutoka suluhu kwenye mchezo wa mpira wa miguu.
Mtendaji wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Simiyu alifunga bonanza hilo kwa kuwashukuru wadau wa Magereza na Uongozi wa Shule ya Sekondari Bariadi kwa ushirikiano waliouonyesha na kuomba kuuendeleza kama sehemu ya kujenga mahusiano mema.
Watumishi wa Mahakama wakiwa katika picha ya Pamoja tayari kwa kuanza bonanza la maadhimisho ya Wiki ya Sheria, 2024.
(Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dodoma)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni