Ijumaa, 26 Januari 2024

WIKI YA SHERIA SINGIDA YAANZA KWA KISHINDO

Na Eva Leshange – Mahakama, Singida 

Mahakama na Wadau wa Haki Jinai mkoani Singida wameungana kuhakikisha wanatoa elimu na msaada wa sheria kwa makundi mbalimbali ili kuhakikisha Wiki ya Sheria inakuwa yenye mafanikio.

Maeneo ya utoaji elimu kwa Singida mjini ni pamoja na Soko Kuu, Soko la matunda Msufini, Stendi ya zamani na Shule ya Sekondari Puma na kwa upande wa Iramba maeneo waliyotoa elimu ni pamoja na Bomani na Soko la Old Kiomboi. 

Wlaya ya Manyoni wao walianza kutoa elimu katika Gereza la Wilaya Manyoni kwa wafungwa na Mahabusu ambao walielezwa haki zao na maboresho ya mifumo kwa sasa yanayoendela mahakamani na kwa namna gani mnyororo wa haki unavyohusisha wadau wengine.

Katika vioski, maswali mengi ambayo watumishi wa Mahakam ana wadau waliyoulizwa na wananchi yalihusiana na mirathi, talaka na ndoa, masuala ya ardhi, matunzo ya watoto na uendeshaji mzima wa mashauri.

Kwa upande wa mashuleni, wanafunzi wamekumbushwa mambo mbalimbali ikiwemo rushwa na athari zake, unyanyasaji wa kingono katika jamii pamoja na makosa ya jinai, na waathirika wakubwa ni wanafunzi, hivyo wanatakiwa kutoa ushirikiano na kuwasilisha taarifa mapema wanapofanyiwa matendo ambayo sio mazuri.

Aidha, wanafunzi hao wamekumbushwa kusoma kwa bidii na kujiepusha na vitendo ambavyo havina maadili.

 Kwa ujumla wiki ya elimu mkoani Singida imepokelewa vizuri huku watumishi na wadau wa Mahakama wakishiriki ipasavyo.

Wananchi wanajitokeza kwa wingi na kufurahia kauli mbiu inayosema, “Umuhimu wa dhana ya Haki kwa ustawi wa Taifa:Nafasi ya Mahakama na wadau katika kuborehsa mfumo jumuishi wa Haki Jinai.” 

Wamesisitiza kufanya kazi kama kaulimbiu invyojieleza ili kuondokana na dhana ya urasimu katika Taasisi za Haki Jinai.

Afisa wa Mahakama, Bw. Lawi Joasi (mbele kushoto) akimsikiliza mwananchi akiuliza maswali mbalimbali kuhusiana na huduma za Kimahakama wakati wa Maonesho ya Wiki ya Sheria.


Sehemu ya wanachi waliofika kupata huduma ya elimu ya sheria katika banda la Mahakama lililopo Soko la Matunda Msufini.

Afisa Kutoka TAKUKURU Wilaya ya Ikungi, Bi. Rashda Mfaume aliyesimama mbele akitoa elimu ya masuala ya rushwa na athari zake kwa wanafunzi wa Sekondari Puma. Aliyeketi pembeni yake ni Hakimu Mahakama ya Mwanzo Ikungi, Mhe. George Mbanguka.

Wadau 
wa Haki Jinai Wilayani Iramba wakitoa elimu katika soko la Samaki Old Kiomboi na aliyeketi mbele katikati  Hakimu Mahakama ya Mwanzo Kiomboi  Mjini, Mhe. Rehema Uroki akitoa mada ya ufunguaji wa mashauri kwa njia ya ki-elecktroniki na namna inavyuhusisha wadau wake.

(Habari hii imehaririwa na Mary Gwera, Mahakama-Dodoma)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni