Na. Eva Leshange, Mahakama Singida
Mahakama na Wadau wa Haki Jinai mkoani hapa hivi karibuni wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria walitembelea Kituo cha Kulelea Watoto Upendo kilichopo Manguanjuki na kutoa msaada wa mahitaji mbalimbali kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
Wadau walioambatana na Mahakama ni pamoja na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, TAKUKURU, Polisi, Mawakili wa Kujitegemea, Ustawi wa Jamii, Magereza na Watu wa Msaada wa Kisheria (Paralegals)
Kituo cha Upendo kilianzishwa mwaka 2008, lengo kubwa nikuwasiaidia watoto wa mitaani wenye mazingira magumu. Watoto hawa wamekuwa wakipatiwa hudumu za elimu, chakula, malazi, bima ya afya, ushauri nasaha na kujengwa kiimani.
Aidha kituo hiki kimefanikiwa kulea watoto hadi kuwafikisha vyuo vikuu na wamekuwa wakifundishwa pia kazi za mikono kama kilimo, ufumaji, ufugaji, ushonaji na kuchomelea.
Akitoa taarifa fupi, Mkurugenzi wa Kituo, Bw. Jackson Kivuyo alisema, “Tunatamani kituo hiki kingesaidia watoto wengi ila changamoto za kupanda kwa gharama za maisha, mfumuko wa bei umemefanya kuwa na wototo 45 tu”.
Aidha kituo kwa sasa kilikuwa na changamoto ya upungufu wa chakula na mahitaji madogo madogo kama mafuta ya kupaka na mengine.
Akikabidhi msaada huo, Mwenyekiti wa Kamati ya Hisani, Mhe. Allu Nzowa altaja mahitaji ambayo wamekabidhi ni unga wa ngano, mchele, sukali, mafuta ya kupikia, taulo kwa watoto wa kike na sabuni za kufulia, ikiwa ni ishara ya upendo na kuwathamini.
Nao Watoto waliwashukuru kwa msaada huo na kutoa hati ya shukrani kwa kuwakumbuka na kurejesha tabasamu lao.
Mahakimu kutoka Mahakama za Mwanzo na Mahakama za Wilaya Singida na watumishi rengaine wa Mahakama wakiwa katika Kituo cha Upendo.
(Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dodoma)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni