Jumanne, 30 Januari 2024

MAHAKAMA, WADAU PWANI WATOA ELIMU GEREZA LA MAHABUSU MKUZA

Na. Eunice Lugiana – Mahakama, Pwani

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kibaha mkoani Pwani pamoja na wadau wametembelea gereza la Mkuza kwa ajili ya kutoa elimu ya sheria wakiwa katika gereza hilo wametoa elimu ya mfumo wa haki jinai kwa kufafanua kauli mbiu ya mwaka 2024 inayohusu kuboreshaji wa mfumo wa haki Jinai.


Akiongea wakati wa elimu hiyo Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Pwani Mhe. Joyce Mkhoi amesema mfumo wa haki jinai kwa Mahakama unaanza tu pale tunapopokea hati ya mashtaka mpaka pale maamuzi yanapotolewa. 


Mhe. Mkhoi amesema kutokana na mfumo huo baadhi ya wadau wanasomana katika mfumo huo kufanya kazi ya kusikiliza mashauri kumaliza kwa wakati ukilinganisha na kipindi cha nyuma.


Akitoa elimu katika gereza hilo Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SP. Betseba Kasanga  amesema kazi ya Polisi  ni kuzuia uharifu kabla haujatokea  ikitokea umetoka jukumu lao pia ni kukamata hivyo jeshi la polisi limekua likitoa elimu kwa mwananchi ili wajue haki zao na kuepukana na vitendo vya kijinai. 


Akiongea pia kwa niaba ya Mkuu ya Mashtaka Pwani Mwanasheria wa Serikali Bi. Aurelia Makundi amesema, mfumo wa haki jinai unaanza kwenye upelelezi kukamata kupeleka mahakamani mpaka kupatikana kwa hukumu. Amesema Mahakama ndiyo chombo kinachotoa haki lakini kikisaidiwa na wadau ambao ni ofisi ya Taifa ya Mashitaka na Polisi. 


Bi. Makundi amesema mfumo wa ofisi ya Mashitaka Taifa umekamilika  na umeunganishwa na Mahakama na leo hii umeanza kufanya kazi  hivyo Mahakama  Pwani na Ofisi ya Mashtaka Pwani wanasomana kwenye mfumo  isipokua polisi ambapo mchakato unaendelea. Amesema nyaraka zote zitapatikana  kwenye mfumo  na hivyo kuepuka ucheleweshaji wa kesi maana hata viongozi wataona kesi imekwama wapi na kushughulikia kwa wakati  pasipo  kusubiria malalamiko kutoka kwa wananchi. 


Wakitoa maoni yao mahabusu wa gereza la Mkuza wameipongeza Mahakama ya Tanzania kwa kufanya kazi kwa bidii na kuweka mifumo ambayo inasaidia kumaliza kesi kwa haraka. wasema haki jinai wamekuwa  wakiiona mahakamani na Magereza maana huko wanafuata sana utaratibu.


Aidha, mahabusu hao wameomba kufanyike marekebisho kwenye sheria ili maelezo ya mtuhumiwa anapotoa akiwa polisi yawe na sahihi tatu yaani mtuhumiwa mwenyewe ndugu yake au wakili na Polisi hiyo itasaidia haki jinai kutendeka kwa uwazi na kuepuka ucheleweshaji wa kesi kwa kukataa maelezo aliyotoa polisi kwamba hakuyatoa kwa uhuru na hivyo kuanza kusikiliza kesi ndogo inapelekea kesi ya msingi kusimama kwa muda.

Hakimu Mkazi Mfawidhi Wa Mahakama Ya Hakimu Mkazi Kibaha mkoani Pwani Mhe. Joyce Mkhoi (wa tatu kushoto) na Mkuu Wa Gereza La Mahabusu Mkuza Mrakibu Wa Magereza Ibrahim Nyamka (wa nne kushoto) wakiwa kenye picha ya pamoja na Wadau Wa Mahakama Kibaha walipofika gerezani hapo kutoa elimu wiki ya sheria.

Hakimu Mkazi Mfawidhi Wa Mahakama Ya Hakimu Mkazi Kibaha Mhe. Joyce Mkhoi Akisalimiana Na Mkuu Wa Gereza La Mahabusu Mkuza Mrakibu Wa Magereza Ibrahim Nyamka Alipowasili Gerezani Hapo Kutoa Elimu.



 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni