Jumanne, 9 Januari 2024

MTUMISHI WA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI SHINYANGA AFARIKI DUNIA

Marehemu Stella Alfred Msilu enzi za uhai wake.

TANZIA

Mahakama ya Tanzania inasikitika kutangaza kifo cha Mtumishi wake Stella Alfred Msilu aliyekuwa akihudumu Mahakama ya Hakimu Mkazi Shinyanga katika Kada ya Mlinzi.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga, Bi. Mavis Miti, marehemu Stella alifikwa na umauti usiku wa kuamkia leo tarehe 09 Januari, 2024 katika hospitali ya Rufaa  Bugando Mwanza ambapo alikuwa amelazwa akipatiwa matibabu. 

Amesema kwa sasa taratibu za mazishi zinafanyika.

Mahakama ya Tanzania inaungana na ndugu, jamaa na marafiki kuomboleza msiba 

Bwana ametoa na Bwana ametwaa, Jina lake lihimidiwe.





Hakuna maoni:

Chapisha Maoni