Jumamosi, 27 Januari 2024

SPIKA WA BUNGE AZINDUA RASMI WIKI YA SHERIA KITAIFA DODOMA

Na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dodoma

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, Mhe. Dkt. Tulia Ackson leo tarehe 27 Januari, 2024 ameongoza wananchi wa Mkoa wa Dodoma katika metembezi maalum kuzindua Wiki ya Sheria inayofanyika kitaifa jijini hapa.

Mhe. Dkt. Tulia aliwasili katika Viwanja vya Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Dodoma, eneo yalipoanzia matembezi hayo majira ya saa 12:15 asubuhi na kupokelewa na mwenyeji wake, Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma.

Baada ya kusalimiana na wananchi, Spika wa Bunge aliungana na Viongozi mbalimbali waliokuwepo katika eneo hilo, akiwemo Jaji Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Khamis Ramadhan Abdalla, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Mohamed Siyani, Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Prof. Elisante Ole Gabriel.

Matembezi hayo yalipitia maeneo ya Polisi, Kanisa Katoliki, Mirembe, Njia Panda ya Iringa na Singida, Sokoni, Uwanja wa Jamhuri na kumalizikia katika Viwanja vya Nyerere Square. Baada ya kufika katika lango la kuingilia, Viongozi hao walifanya mazoezi kidogo ili kupasha viungo na kuuweka mwili sawa.

Baadaye, Jaji Mkuu alimwongoza Mgeni Rasmi kutembelea mabanda ya maonesho ya Wiki ya Sheria ambayo yameandaliwa na Mahakam ana wadau mbalimbali katika Viwanja hivyo, ambapo alijionea kazi zinazotolewa katika muktadha mzima wa utoaji haki nchini.

Miongoni mwa mabanda aliyotembelea ni la Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), Kurugenzi ya Menejimenti ya Mashauri na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), Mahakama ya Afrika Mashariki na Wizara ya Katiba na Sheria.

Viongozi wengine walioshiriki katika matembezi hayo ni Majaji wa Mahakama ya Rufani, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Kaimu Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Naibu Wasajili, Watendaji na wengine wengi.

Baada ya kutembelea mabanda hayo, Spika wa Bunge na Viongozi Wakuu walielekea kwenye Jukwa Kuu ambapo Wimbo wa Taifa ulipigwa kabla ya Mshereheshaji wa shughuli hiyo, Kaimu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Projestus Kahyoza kuendelea na ratiba nyingine.

Kaulimbiu ya Wiki na Siku ya Sheria ya mwaka huu 2024 ni “Umuhimu wa Dhana ya Haki kwa Ustawi wa Taifa: Nafasi ya Mahakama na Wadau Katika Kuboresha Mfumo Jumuishi wa Haki Jinai.”

Kilele cha Maonesho ya Wiki ya Sheria kitafanyika tarehe 1 Februari, 2024 katika Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akisalimiana na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma baada ya kuwasili kwenye Viwanja vya Kituo Jumuishi vya Utoaji Haki Dodoma kabla ya kuanza kwa matembezi maalum kuzindua rasmi Wiki ya Sheria nchini.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (katikati) akiwa na Viongozi wengine wakati wa kuanza matembezi hayo.

Majaji wa Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu ya Tanzania wakishiriki matembezi hayo. Picha chini inaonesha Watumishi wa Mahakama katika matembezi hayo maalum.



Wadau mbalimbali wa Mahakama wakiwa kwenye matembezi hayo yanayoongozwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, Mhe. Dkt. Tulia Ackson.




Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (katikati) na Viongozi wengine wakikatisha mitaa wakati wa matembezi hayo.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, Mhe. Dkt. Tulia Ackson na Viongozi wengine (juu na chini) wakipasha mbele ya lango la kuingilia kwenye Viwanja vya Nyerere Square baada ya kushiriki matembezi hayo maalum.



Pasha pasha ikiendelea (juu na chini).


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, Mhe. Dkt. Tulia Ackson na Viongozi wengine wakiwa katika banda la Kurugenzi ya Menejimenti ya Mashauri. Picha chini wakiwa katika banda la Wadau wa Haki Jinai.


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akipokea zawadi alipotembelea banda la Mahakama ya Afrika Mashariki.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, Mhe. Dkt. Tulia Ackson na Viongozi wengine wakiwa katika banda la Mamlaka ya Kuthibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya. Picha chini Viongozi hao wakiwa kwenye banda la Wizara ya Katiba na Sheria.



Meza Kuu ikiongozwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, Mhe. Dkt. Tulia Ackson ikishiriki kuimba Wimbo wa Taifa baada ya kutembelea mabanda ya maonesho ya Wiki ya Sheria.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni