Na. Stephen Kapiga-Mahakama, Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Amosi Makala ametembelea viwanja vya Furahisha jijini hapo leo tarehe 24 Januari, 2024 kujionea huduma mbalimbali za kisheria zinazotolewa na Mahakama na Wadau na kuwasisitiza viongozi wa kiserikali kuwahimiza wananchi kufika katika viwanja hivyo kupata elimu ya sheria inayotolewa kwa muda wa wiki nzima ili kupunguza malalamiko Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Akiambatana na Kamati ya Usalama ya Mkoa wa Mwanza, Mhe. Makala alijionea jinsi maandalizi mbalimbali yalivyokamilika ikiwa ni pamoja na kutoa namna ya kuboresha baadhi ya maeneo katika uwanja huo ili kuwezesha wananchi kupata elimu ya sheria wakiwa katika mazingira salama na ya usafi.
Aidha, Mhe Makala aliwasihi viongozi wengine walioambatana naye kuhakikisha kuwa wanawasisitiza wananchi katika maeneo yao wafike katika viwanja vya furahisha ili kuweza kupatiwa elimu ya sheria na kama wakielewa basi malalamiko yahusiyo sheria katika ofisi yake yatapungua kwa kiasi kikubwa na hivyo kuondokana na malalamiko ambayo yanaweza kupatiwa ufumbuzi kwa njia elimu ya sheria itakayo tolewa kwa muda wa wiki.
“Nakuagiza Katibu Tawala mkoa kuhakikisha kuwa usafi wa mazingira unafuatiliwa kwa umakini sana kwani tunajua kwa sasa kuna wimbi la ugonjwa wa kipindupindu katika baadhi ya maeneo ndani ya Mkoa wetu hivyo hakikisha kuwa usafi unazingatiwa kwa watu wote watakaofika eneo hili kupata elimu ya sheria kwa kipindi cha wiki nzima” alisema Mkuu wa Mkoa
Mbali
na Mahakama ya Tanzania, Wadau wengine wanaoendelea na zoezi la utoaji wa elimu ya sheria
katika viwanja vya Furahisha jijiji Mwanza ni pamoja na Idara ya Uhamiaji, Jeshi
la Magereza, Jeshi la Polisi (Tanpol), Ofisi ya Taifa ya Mashitaka, Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Kamishina wa Ardhi, Chama chaa Wanasheria
Tanganyika (TLS), Umoja wa Madalali wa Mahakama Mkoa wa Mwanza, Taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Idara ya Misitu, Idara ya Uvuvi,
Idara ya Wanayama Pori, na Wadau wengine kama Taasisi za Kifedha.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza
Mhe Amosi Makalla (katikati mstari wa wanaotembea) akiwasili kwenye maeneo ya mabanda ya kutolea elimu ya wiki ya sheria katika
viwanja vya furahisha ili kujionea kinachoendelea katika viwanja hivyo ikiwa ni
siku ya kwanza ya wiki ya sheria Nchini maonesho yameanza leo tarehe 24 Januari,
2024 katika viwanja vya Furahisha Jijini Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa
Mwanza Mhe. Amosi Makalla (aliyenyanyua mikono) akizungumza na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Mwanza
akiwa katika viwanja vya furahisha Jijini mwanza alipotembelea viwanja hivyo
kujionea maendeleo ya wiki ya sheria Nchini iliyoanza rasmi leo tarehe 24
januari 2024 nchini kote.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni