Jumatano, 31 Januari 2024

WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA MBOZI WANUFAIKA NA ELIMU YA SHERIA

Na Iman Mzumbwe-Mahakama, Songwe

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Hakimu Mkazi Songwe, Mhe, Hassan Makube, Mtendaji wa Mahakama na Wadau jana tarehe 30 Januari, 2024 waliwatembelea Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya Mbozi kuwapa elimu ya sheria iliyokuwa inatolewa ndani ya kipindi cha Wiki ya Sheria mkoani hapa.

natolewa Mkoani humo katika wiki hii sheria. 

Wadau walioungana na Hakimu Mkazi Mfawidhi ni Ofisi ya Taifa ya Mashitaka, Mawakili wa Kujitegemeana, Afisa wa Huduma kwa Jamii na Dawati la Jinsia (police desk) huku maada zilizoandaliwa na kutolewa ni mirathi na wosia, unyanyasaji wa kijinsia, Mahakama ya Watoto na utaratibu wake na elimu ya kifungo cha nje kwa walio na sifa.

Mtendaji wa Mahakama alielezea mpango mkakati wa mahakama wa mwaka 2020/2021-2024/25 pamoja na mambo mengine unalenga kuchangia kufikia malengo ya dira ya taifa ya maendeleo 2025.

Kadhalika, alieleza kuwa mamlaka ya Mahakama yanatokana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, chini ya Ibara ya 107A na ile ya 107B, kwamba Mahakama ndiyo chombo chenye mamlaka ya mwisho ya maamuzi katika kutoa haki na kuleta amani nchini kwa kwa kuzingatia Katiba na Sheria ya nchi.

Naye Afisa kutoka Dawati la Kijinsia ametoa elimu ya unyanyasaji wa kijinsia kwa watumishi hao akisema kuwa unyanyasaji wa kijinsia unaweza kukatisha ndoto ya mtu, hivyo akawasihi wadau hao kuripoti sehemu husika mara baada wanapoona vitendo hivyo vya kikatili vinapotokea katika jamii.

Kwa upande wake, Hakimu Mfawidhi Mahakama ya Wilaya Mbozi, Mhe. Nemes Chami alieleza jinsi Mahakama ya Watoto inavyofanya kazi na jinsi mtoto anavyopata haki zake akiwa mahakamani.

Aliwasihi wadau hao kuwa walezi bora kwa watoto na kukemea tabia mbaya ili kuepukana na vitendo viovu, kwani hatua hiyo itasaidia watoto kuwa na malezi mazuri.

Afisa Tarafa kutoka Itaka ambaye alimwakilisha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi aliishukuru Mahakama kwa kazi nzuri wanayoifanya kwa wanachi kwa kutoa elimu ya sheria, kwani imesaidia watu wengi kuwa na ufahamu juu ya masuala ya kisheria katika jamii.

Alipendekeza kama ikiwezekana Mahakama iongeze muda wa kutoa elimu kwa wananchi kutoka Wiki moja hadi Wiki mbili kwa mwaka unaofuata ili elimu hiyo iwafikie watu wengi zaidi katika jamii.


Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Hakimu Mkazi Songwe, Mhe, Hassan Makube (kushoto) akiwa na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, Bw. Rashid Mwaisaka.

Mtendaji wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Songwe akielezea mpango makakati wa Mahakama.

Afisa kutoka Dawati la kijinsia akitoa elimu ya unyanyasaji wa kijinsia kwa wadau.

Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Mbozi, Mhe. Nemes Chami akitoa elimu juu ya Mahakama ya Watoto na utaratibu wake.

Afisa wa huduma kwa jamii, Bw. Francis citojo akieleza namna wavyotoa huduma kwa watu ambao wana sifa za kuwa katika kifungo cha nje.

Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya Mbozi wakisiliza elimu inayotolewa.

(Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Dodoma)

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni