Jumatatu, 29 Januari 2024

WIKI YA SHERIA YANOGA SONGWE

Na Iman Mzumbwe-Mahakama, Songwe

Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya, Mhe. Emmanuel Kawishe leo tarehe 29 Januari, 2024 amefanya ziara ya kikazi mkoani Songwe na kujionea shughuli za utoaji elimu katika Wiki ya Sheria na kuridhishwa na zoezi hilo.

Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mhe. Hassan Makube amemueleza Mhe Kawishe kuwa jumla ya shule 29 za Sekondari na Msingi zilizopo mkoani Songwe zinatembelewa katika Wiki ya Sheria, huklu utoaji elimu ukifanyika pia katika maeneo ya wazi, redioni na maeneo yote ya Mahakama.

Jaji Kawishe ametembelea pia Shule ya Sekondari Nambala iliyopo Wilaya ya Mbozi kujionea shughuli za utoaji elimu katika Wiki ya Sheria na kuwahimiza Wanafunzi kutojihusisha na matendo maovu.

“Elimu mnayopatiwa katika wiki hii ni muhimu katika ukuaji wenu na hakikisheni mnanufaika na kuwa na maadili mema shuleni pamoja na majumbani, pia mtangulizeni Mungu katika masomo yenu na hakika elimu ndio ukombozi wenu,” Jaji Kawishe amewaeleza Wanafunzi hao.

Kadhalika, Jaji Kavishe ametembelea mradi wa ujenzi wa Ktuo Jumuishi (MINI IJC) na kuipongeza Mahakama ya Tanzania katika kuboresha miundombinu ya Mahakama na kuwasogezea huduma karibu wananchi. Amesema kua kituo hicho kitapunguza kero kwa wananchi katika kufuata huduma za Mahakama Kuu Mbeya.

Katika Ziara hiyo Jaji kavishe ameambatana na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Mbeya, Mhe. Aziza Temu ambaye pia ameipongeza Mahakama ya Hakimu Mkazi Songwe kwa kufanya kazi nzuri ya utoaji elimu kwa wananchi, wanafunzi na wadau mbalimbali wa Mahakama.


Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya, Mhe. Emmanuel Kawishe akipokea taarifa ya Wiki ya Sheria.

Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mhe. Hassan Makube akiwasilisha taarifa ya utendaji ya Wiki ya Sheria.

Naibu Msajili Mahakama Kuu Mbeya, Mhe. Aziza Temu akisiliza taarifa ya utoaji elimu Wiki ya Sheria.

Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya, Mhe. Emmanuel Kawishe baada ya kuwasili katika Shule ya Sekondari Nambala.

Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya, Mhe. Emmanuel Kawishe akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nambala.

Naibu Msajili Mahakama Kuu Mbeya, Mhe. Aziza Temu akiwaaga Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nambala.

Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya, Mhe. Emmanuel Kawishe akiwa katika Mradi wa Ujenzi wa Kituo Jumuishi Mkoa wa Songwe.

(Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dodoma)

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni