Na. Richard Matasha – Mahakama, Mtwara
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya
Mtwara, Mhe. Rose Ebrahim akihutubia amesema Mahakama pamoja na wadau wake wote
wanawajibika kuhakikisha haki inapatikana kwa wakati na kwa wote, kwa kutumia
mifumo ya TEHAMA ipasavyo kwa kiasi kikubwa kufikia malengo ya Taasisi
iliyojiweke.
Akitoa hotuba yake katika kilele cha maadhimisho ya
siku ya sheria nchini inayoashiria kuanza kwa mwaka mpya wa kimahakama jana
tarehe mosi Februari, 2024 Mhe. Ebrahim alisema ni wajibu wa Mahakama na wadau
kuhakikisha mifumo kitehama inayoratibu mnyororo wa haki jinai na mashauri kwa
ujumla ikasomana kutoka taasisi moja hadi nyingine ili mwananchi aweze
kuhudumiwa kwa haraka na kwa wakati.
Naye, Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba, Kanali. Patrick Sawala ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mtwara amepongeza juhudi kubwa za maboresho yanayofanyika katika ngazi zote za Mahakama na kusisitiza wadau wengine kuongeza kasi ili kufikia malengo ya pamoja ya kutoa haki kwa kwa wananchi kwa wakati ili kuimarisha Imani ya Mahakama kwa wadau wake.
Katika maadhimisho hayo watumishi wanne wa Mahakama wamezawadiwa zawada za vyeti vya pongezi kwa kuthibitika kuwa ni watumishi waliofanya kazi kwa weledi, uwajibikaji na nidhamu ya hali ya juu. Imekua ni desturi ya Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara kuwazawadia watumishi wenye utumishi uliotukuka.
Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara Mhe. Rose
Ebrahim, aliambatana na viongozi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara ambao ni
Majaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara Mhe. Martha Mpaze na Mhe Saidi Ding’ohi,
Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara, Mhe Seraphine Nsana, Mtendaji wa
Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara Bw. Richard Mbambe, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya
Hakimu Mkazi Mtwara Mhe Charles Mnzava pamoja na watumishi wengine katika
kuadhimisho siku ya sheria nchini.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara, Mhe. Rose Ebrahim
akihutubia hadhara ya wananchi na wadau wa Mahakama (hawapo pichani) iliyojitokeza katika maadhimisho ya siku ya sheria.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara, Mhe. Rose Ebrahim (wa pili kusho) akiwa ameambatana na Majaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara, Mhe. Saidi Ding’ohi (Kushoto), Mhe. Martha Mpaze (Kulia) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba, Kanali, Patrick Sawala (mwenye kaunda suti) wakiingia katika viwanja vya Mahakama Kuu Mtwara.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara, Mhe. Rose Ebrahim (wa pili kushoto),
Majaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara, Mhe. Saidi Ding’ohi (Kushoto) na Mhe.
Martha Mpaze (Kulia) wakiwa wameketi meza kuu pamoja na Mkuu wa Wilaya ya
Tandahimba, Kanali, Patrick Sawala (wa pili kulia) wakati wa maadhimisho ya siku ya sheria nchini yaliyofanyika katika viwanja vya Mahakama Kuu Mtwara.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara, Mhe. Rose Ebrahim akikagua gwaride lililoandaliwa na kikosi mahiri cha askari polisi mkoani Mtwara wakati wa maadhimisho ya siku ya sheria.
Sehemu ya watumishi wa Mahakama na wadau wakifuatilia hotuba ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara, Mhe. Rose Ebrahim katika maadhimisho ya siku ya sheria mkoani Mtwara.
Mmoja kati ya watumishi wanne waliozawadiwa vyeti vya pongezi, Bw. Julius Nhelegani akipokea cheti kwa utumishi uliotukuka ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya sheria mkoani Mtwara kutoka kwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara, Mhe. Rose Ebrahim.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni