Na Evelina Odemba – Mahakama, Morogoro
Ikiwa ni wiki takribani tatu zimepita tangu kuadhimishwa kilele cha wiki ya sheria Kanda ya Morogoro na kote Nchini, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Morogoro, Mhe. Latifa Mansoor amekutana na watumishi ili kufanya tathimini na kupeana mikakati.
Akizungumza katika kikao hicho, Mhe. Mansoor aliwapongeza watumishi hao wa Mahakama kwa kujitoa kwao kuwajibika katika majukumu waliyokabidhiwa ili kuhakikisha maadhimisho yanafana.
“Niwapongeze Majaji Kanda ya Morogoro, watendaji na watumishi wenzangu, hakika mmefanya kazi kubwa na nzuri, naamini baada ya hapa tutaenda kujipanga vyema ili wiki ya sheria ijayo kusiwepo na changamoto zilizobainishwa hapa,” alisema.
Aidha, Jaji Mansoor alisisitiza suala la uwajibikaji kwa kila mtumishi wa Mahakama na kueleza kuwa inawapasa kuwa na ushirikiano, umoja na
uwajibikaji.
Aliongeza kuwa kila mtumishi yupo kwa jukumu moja kubwa la kumuhudumia mwananchi kwa usahihi na kwa wakati ili kuhakikisha wanaipeperusha vyema bendera ya Mahakama ya Tanzania kote nchini.
“Kila mmoja wetu hapa anatakiwa kuufahamu vyema mpango makakati wa Mahakama na kuuishi, tukifanya hivyo wote tutakwenda sambamba na dira ya
Mahakama inavyotutaka.
“…mtumishi yeyote atakayekwenda kinyume na maadili hatofumbiwa macho kwa kuwa atakuwa anatukwamisha kufikia marengo yetu tuliyojiwekea sisi kama Mahakama kupitia mapango makakati wetu,” alihitisha Mhe. Mansoor.
Naye Naibu Msajili Mfawidhi, Mhe. Fadhili Mbelwa alipata wasaa wa kuwapitisha watumishi hao katika baadhi ya vipengele vya Mpango Mkakati wa Mahakama.
Aligusia kuwa maboresho makubwa yanayoonekana yamefanywa ni sehemu ya mkakati huo, hivyo kila mtumishi ana wajibu wa kuunga mkono kwa kuhakikisha anatekeleza majukumu yake kwa haki na usawa na kwa wakati.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Morogoro, Mhe. Latifa
Mansoor akizungumza wakati wa kikao na watumishi wa Mahakama (hawapo pichani).
Kutoka katika kikao cha watumishi wa Mahakama Kanda ya Morogoro kulia ni
Jaji Mfawidhi, Mhe. Latifa Mansoor, kushoto ni Jaji wa Mahakama Kuu, Mhe. Hadija Kinyaka na aliyekaa kwa mbele ni Naibu Msajili, Mhe. Fadhili Mbelwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni