Na. Stephen Kapiga-Mahakama, Mwanza.
Jaji
Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahimu Hamis Juma tarehe 15 Februari 2024 aliwaongoza
Majaji wa Mahakama ya Rufaa ya Tanzania wanaondelea na vikao vya Mashauri ya
Mahakama ya Rufani katika zoezi la upandaji miti ya matunda katika eneo la
viwanja vya jengo la Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Jijini Mwanza.
Mhe. Prof. Juma katika zoezi hilo aliongozwa na mwenyeji wake Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mwanza Mhe.Dkt Ntemi Kilekamajenga pamoja na watumishi wa Mahakama wanaofanya kazi katika jengo la Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki jijini Mwanza na kupanda jumla ya miti sita ya matunda katika zoezi hilo.
“Nimefurahi
kuweza kushiriki katika zoezi hili kwani naamini miti ni moja ya kumbukumbu
nzuri inayoishi, nawasihi sana muweze kupanda miti kwa wingi katika maeneo yenu
kwani ni moja ya njia ya utunzaji wa mazingira katika maeneo yetu ya kazi hata
majumbani”, alisema Mhe.Prof. Juma.
Katika
upandaji miti huyo uliwashirikisha Majaji wa Mahakama ya Rufani walioko katika vikao
vya usikilizaji wa mashauri ya Mahakama ya Rufani Kanda ya Mwanza ambao ni Jaji
wa Rufani ya Tanzania, Mhe. Rehema Mkuye, Mhe. Dkt. Mary Levira, Mhe. Lameck Mlacha,
Mhe. Paul Ngwembe na Mhe. Abrahamu Mwampashi.
Waheshimiwa
Majaji hao, wanaendelea na vikao vya kusikiliza mashauri ya Mahakama ya Rufani katika
Mahakama ya Rufani ya Tanzania masijala ndogo ya mwanza ambapo jumla ya Mashauri
78 yanatarajiwa kusikilizwa na kutolewa uamuzi na kati ya Mashauri hayo
Mashauri ya jinai ni 16, Mashauri ya madai ni 16, Mashauri ya maombi ya madai
ni 44 na Mashauri ya maombi ya jinai ni 2.
Vikao
hivyo vinatarajiwa kufikia tamati siku ya tarehe 23 Februari, 2024 na hivyo
kuendelea na kasi ya uamuzi wa mashauri katika Mahakama ya Rufani ya Tanzania
kwa lengo la kuendana na mpango mkakati wa Mahakama ya Tanzania wa mwaka
2020/2021-2024/2025 hasa katika nguzo yake ya pili ya kuhakikisha kuwa
upatikanaji wa haki kwa wakati na kwa wote.
Jaji Mkuu Tanzania Mhe. Prof. Ibrahimu Hamis Juma akipanda mti wa matunda ya
machungwa kama kumbukumbu katika eneo la kituo jumuishi cha utoaji haki Jijini
mwanza zoezi lilifanyika tarehe 15 februari 2024.
Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania Mhe. Rehema Mkuye akipanda mti wa matunda ya machungwa kama kumbukumbu katika eneo la kituo jumuishi cha utoaji haki Jijini Mwanza.
Jaji wa Mahakama
ya Rufani ya Tanzania Mhe. Dkt. Mary Levira akipanda mti wa matunda ya mparachichi
kama kumbukumbu katika eneo la kituo jumuishi cha utoaji haki Jijini mwanza.
Jaji wa Mahakama
ya Rufani ya Tanzania Mhe. Dkt. Mary Levira akipanda mti wa matunda ya mparachichi
kama kumbukumbu katika eneo la kituo jumuishi cha utoaji haki Jijini mwanza.
Jaji wa Mahakama
ya Rufani ya Tanzania Mhe. Abraham Mwampashi akipanda mti wa matunda ya
machungwa kama kumbukumbu katika eneo la kituo jumuishi cha utoaji haki Jijini
mwanza.
Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania Mhe. Abraham Mwampashi akipanda mti wa matunda ya machungwa kama kumbukumbu katika eneo la kituo jumuishi cha utoaji haki Jijini mwanza.
Jaji wa Mahakama
ya Rufani ya Tanzania Mhe. Lameck Mlacha akipanda mti wa matunda ya mparachichi
kama kumbukumbu katika eneo la kituo jumuishi cha utoaji haki Jijini mwanza.
Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania Mhe. Paul Ngwembe akipanda mti wa matunda ya mparachichi kama kumbukumbu katika eneo la kituo jumuishi cha utoaji haki Jijini mwanza
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni