Ijumaa, 2 Februari 2024

TUFUNGAMANE NA MIFUMO YA MAHAKAMA KATIKA KUTOA HAKI – JAJI MANSOOR


Na Evelina Odemba – Mahakama Morogoro

 Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Morogoro Mhe. Latifa Mansoor atoa rai kwa wadau wa Haki kufungamana na mifumo ya Mahakama ili kurahishisha jukumu zima la utoaji haki.

 Mhe. Mansoor aliyasema hayo wakati akitoa hotuba kwenye kilele cha siku ya sheria Nchini leo tarehe 1 Februari, 2024 ambapo kwa kanda ya Morogoro maadhimisho hayo yalifanyika katika viwanja vya Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki kilichopo Manispaa ya  Morogoro.

“Naomba nipongeze hatua kubwa zilizopigwa na Mahakama ya Tanzania katika matumizi ya mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA kama nilivosema hapo awali, hatua hizo zitumike kama chachu ya ofisi zingine za wadau kuongeza nao jitihada na kasi ya kuanza kutumika kwa mfumo hii na maanisha mifumo hii ifanye kazi shirikishi , yaani tufungamane katika kutoa haki ili kuwe na mantiki ya haki kwa wakati” alisisitiza Mhe. Mansoor.

Aidha Mhe. Jaji Mansoor aliendelea kuzitaka taasisi zingine za uchunguzi kuanzisha TEHAMA itakayosaidia kufuatilia mwenendo na vielelezo vitakavyowasilishwa Mahakamani        pamoja na uendeshaji wa vielelezo ambavyo Mahakama tayari itakuwa imevitumia.

Akiwasilisha salamu za Serikali Naye Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima ambaye alikuwa mgeni maalum wakati wa sherehe za maadhimisho hayo aliwasisitiza  wadau wa Mahakama wasisite kuwa wakali kwenye usimamizi wa sheria kwa wale wote wanaoendelea kutenda vitendo vya ukatili kwenye jamii, huku akionesha kusikitikitishwa na vitendo vya ukatili wa kingono kwa watoto wadogo.

“Nachukizwa  ninapopata taarifa kuwa kuna watu wenye mmomonyoko wa maadilili wanafanya ukatili hasa kwa watoto wadogo, nakemea vikali vitendo hivyo,”.  alieleza Mhe. Malima.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) Baraka Lweeka alisema kuwa endapo mapendekezo yaliyotolewa na tume ya haki jinai yatafanyiwa kazi ipasavyo itasaidia kuwa na taifa zuri lenye kujali na kusimamia misingi ya haki kwa jamii.

Katika sherehe hizo zilihudhuriwa na viongozi mbalimbali ngazi ya mahakama wakiwemo Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Morogoro, Mhe. Amiri Mruma, Mhe. Khadija Kinyaka, Mhe. Devota Kamzola, Upande wa Serikali Mbali na Mkuu wa Mkoa pia alikuwepo Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mhe. Rebeca Nsemwa , Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa na Wilaya, Viongozi wa Dini, wazee, wanasiasa, wadau, watumishi wa Mahakama na wananchi ambapo katika sherehe hizo pia kulipambwa na burudani mbalimbali zilizobeba jumbe zenye kulenga kauli mbiu.

  Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Morogoro Mhe. Latifa Mansoor akihutubia wakati wa sherehe za kilele cha Siku ya Sheria Mkoani Morogoro.

  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima akitoa salamu za serikali katika maadhimisho ya kilele cha Siku ya Sheria Mkoani Morogoro.


  Meza kuu ikiongozwa na mgeni rasmi ambaye ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Morogoro Mhe. Latifa Mansoor (wa tatu mstari wa mbele) (kushoto kwake) ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima, (kulia kwake) ni Jaji Mhe   Amiri. Mruma, (wa kwanza kushoto) ni Jaji Mhe. Devotha Kamzola na wa (kwanza kulia) ni Jaji Mhe. Khadija Kinyaka wakitoa heshima wakati wimbo wa taifa unaimba katika sherehe za kilele cha Siku ya Sheria.

 Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Morogoro Mhe. LatifaMansoor (aliyesimama kwenye jukwaa) akiwa tayari kukagua gwaride la heshima lililopigwa kwake wakati wa sherehe za kilele cha Siku ya Sheria.

   Wakili wa Serikali Mfawidhi Kanda ya Morogoro Mhe. Xavier Ndalawa akitoa salamu toka ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakati wa maadhimisho ya kilele cha Siku ya Sheria .


  Askari toka Jeshi la Polisi Tanzaia wakiwa katika ukakamavu wakati wimbo wa taifa  wakati wa sherehe za kilele cha Siku ya Sheria.

Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Morogoro Mhe. Fadhili Mbelwa akiongoza sherehe ya kilele cha Siku ya Sheria.


   Mwenyekiti wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) Mhe. Baraka Lweeka akitoa salamu za Chama wakati wa maadhimisho ya kilele cha Siku ya Sheria.


Picha ya Meza kuu pamoja na viongozi wa dini na wazee wa Mkoa wa Morogoro.


 Meza kuu pamoja na baadhi ya Wahe. Mahakimu Kanda ya Morogoro.

 

Sehemu ya watumishi na wadau wa Mahakama wakifuatilia matukio wakati wa sherehe  za kilele cha Siku ya Sheria.


    Kwaya ya Mahakama Kanda ya Morogoro ikitumbuiza wakati wa kilele cha        Siku ya Sheria.

   Picha ya pamoja meza kuu na baadhi ya watumishi wa Mahakama wakati wa sherehe za kilele cha Siku ya Sheria.


  Picha ya pamoja ya meza kuu na wadau wa Mahakama wakiwemo waendesha Mashtaka wa Serikali, Mawakili wa Serikali na Mawakili kujitegemea.

 


 

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni