Alhamisi, 7 Machi 2024

BALOZI WA TANZANIA UGANDA AMTEMBELEA JAJI MKUU

Na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Kampala

Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Maj. Gen. Paul Kisesa Simuli leo tarehe 7 Machi, 2024 amemtembelea Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma katika Hoteli ya Mestil jijini hapa na kufanya naye mazungumzo mafupi.

Balozi Simuli aliwasili hotelini hapo majira ya saa 6.45 mchana akiwa ameambatana na Ofisa kutoka ubalozini, Bw. Lucas Mayanga na kuelekea moja kwa moja kwa Jaji Mkuu alipokuwa amefikia.

Ujio wa Balozi huyo wa Tanzania unakuja masaa machache baada ya kumalizika kwa Mkutano wa kKimataifa wa Mahakama Afrika uliokuwa unafanyika nchini Uganda kujadili njia mbadala ya utatuzi wa migogoro, ikiwemo njia ya usuluhishi.

Baada ya kukutana na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Maj. Gen. Simuli alikutana na Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania waliokuwa katika Mkutano huo, Mhe. Zahra Maruma na Mhe. Isaya Arufani na kubadilisha nao mawazo kuhusu masuala mbalimbali ya kiutendaji.

Jaji Mkuu na ujumbe wake wanatarajia kurejelea nchini Tanzania leo tarehe 7 Machi, 2024 baada ya kushiriki Mkutano huo uliokuwa umeandaliwa na Mahakama ya Uganda kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Pepperdine kilichopo California Marekani.


Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Maj. Gen. Paul Kisesa Simuli (kushoto) akisalimiana na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma alipomtembelea leo tarehe 7 Machi, 2024 jijini Kampala. Picha chini Viongozi hao wakiwa katika mazungumzo.


Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Maj. Gen. Paul Kisesa Simuli (katikati) akiwa katika picha ya pamoja naMajaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania waliokuwa katika Mkutano huo, Mhe. Zahra Maruma (kulis) na Mhe. Isaya Arufani (kushoto). Picha chini, Balozi Simuli akizungumza na Majaji hao. Mwenye shati jeupe ni Afisza wa Ubalozi, Bw. Lucas Mayanga.



Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Maj. Gen. Paul Kisesa Simuli akiwa katika picha ya pamoja na Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Watumishi wengine wa Mahakama, Naibu Msajili Mahakama Kuu Kituo cha Usuluhishi, Mhe. Augustina Mmbando (wa pili kushoto) na Afisa Itifaki, Bw. Juma Mshana.












Hakuna maoni:

Chapisha Maoni