Na Magreth Kinabo-Mahakama
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salam,Mhe. Salma Maghimbi amewataka wanawake wa kanda hiyo kuishi kauli mbiu ya Siku ya Wanawake Duniani kwa kuangalia kuanzia ngazi ya familia.
Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 8 Machi na Mhe. Maghimbi wakati kanda hiyo ilipokuwa inaadhimisha siku hiyo kwenye ukumbi namba moja wa Mahakama Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam yenye kauli mbiu ‘Wekeza kwa Wanawake kuharakisha Maendeleo ya Taifa na Ustawi wa Jamii.
“Ni vema tuiishi kauli mbiu hii kwa kuangalia kuanzia ngazi ya familia tunaleaje familia zenu nyumbani, ukiwa mama unaleaje watoto kwa kuzingatia maadili mema, je tunalea watoto wetu kwa kuzingatia usawa,” alisema Jaji Maghimbi.
Jaji Mfawidhi huyo pia alitumia nafasi hiyo kuwaasa wanawake hao kupendana na kuwa na ushirikiano ili kutimiza malengo yaliyokusudiwa katika shughuli zao.
Kwa upande wake Jaji wa Mahakama hiyo, Mhe. Butamo Philip aliwataka wanawake hao,kuwa na tabia ya kuanza kujiwezesha badala kusubiri kuwezeshwa, kwa kuwa ni jambo zuri na kitu kizuri kinaanza nguvu zako.
“Kila mmoja ajitathimini mimi kama mimi ninafanya nini kuanza kujiwezesha ndani ya familia halafu kwa taifa, “ alisisitiza Mhe. Jaji Philip.
Aliongeza kwamba wanapaswa kufanya kazi kwa bidii na umakini kwa vitendo, ikiwemo kujiletea maendeleo.
Naye Jaji wa Mahakama hiyo, Mhe. Elizabeth Mkwizu alisema maandiko matakatifu yanaeleza kuwa mwanamke sio mtu wa kumtegemea mtu, bali ukimwezesha atafanya kila kitu na atazalisha, pia sio mtu wa kununuliwa kila kitu kwani naye anatafuta.Pia aliwaomba wanawake hao kutokuwa kero kwa wanaume zao.
Jaji Mafawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam,Mhe. Salma Maghimbi(katikati mstari wa mbele) akiwa katika pamoja na watumishi wa kanda hiyo.(kushoto) ni Jaji wa Mahakama hiyo,Mhe, Butamo Philip na (Kulia ) ni Mhe. Jaji Elizabeth Mkwizu.
Jaji Mafawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam,Mhe. Salma Maghimbi(katikati mstari wa mbele) akiwa katika pamoja na watumishi wa Masjala Kuu (kushoto) ni Jaji wa Mahakama hiyo,Mhe, Butamo Philip na (Kulia ) ni Mhe. Jaji Elizabeth Mkwizu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni