Jumamosi, 9 Machi 2024

MAHAKAMA MOSHI WAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KWA KUFANYA MATENDO YA HURUMA

Na. Paul Pascal-Mahakama Moshi

Wanawake wa Mahakama Kuu Kanda ya Moshi wameadhimisha siku ya wanawake Duniani leo tarehe 8 march 2024 kwa kutembelea Kituo cha wazee wasiojiweza kilichopo Kata ya Njoro Manispaa ya Moshi Mkoa wa Kilimanjaro na kufanya matendo ya huruma.


Akizungumza katika kituo hicho Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Moshi, Mhe. Dkt. Lillian Mongella amesema “sisi kama wanawake tunao wajibu wakuwajali wazee wetu kwani wazee ni hazina ya Taifa. Niwasisitize na kuwaasa wanawake wenzangu tuwe na utamaduni wa kutoa kile kidogo tunachokipata kuwakumbuka wazee wetu haswa wazee wasiojiweza kama tunalivyofanya leo...


Tujiwekee utaratibu endelevu wa kuwajulia hali, kuwapatia mahitaji muhimu kadiri tunavyojaaliwa ili nao waone furaha yakuwa katika ulimwengu huu, ni wajibu wetu kama wanawake kuwatunza wazee wetu katika jamii.” Amesisitiza Mhe. Mongella.


Naye, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Moshi Mhe. safina simfukwe amesema, “nipongeze uratibu uliofanyika wa kufanikisha jambo hili hakika tumechagua fungu lililo jema, tumewapa faraja wazee wetu kwa hiki tulichojaaliwa niushukuru uongozi wa kituo hichi kwa juhudi zao za kuwahudumia wazee hawa wasiojiweza pia niombe zoezi hili liwe endelevu,” ameongeza Mhe. Jaji.


Kwa upande wake, Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Moshi Mhe. Sekela Mwaiseje amesema “kuwajali na kuwatunza wazee ni Ibada hakika leo siku ya wanawake tumefanya jambo tunalopaswa kulienzi nakulitekeleza kila tunapojaaliwa niwaombe wanawake wote jambo hili tuliendeleze mara kwa mara”


Aidha, Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Moshi Bi. Maria Itala amebainisha kuwa katika siku ya wanawake wamefanikiwa kuwapatia wazee wa kituo cha njoro vifaa vya matumizi ya kila siku pamoja na nafaka kwa ajili ya vyakula vyao vyote hivyo vikiwa vimepatikana kupitia michango ya wanawake wa Mahakama Kuu Kanda ya Moshi waliojichanga.

Kituo cha wazee wasiojiweza Njoro kina jumla ya wazee 18 ambapo 12 kati yao ni wanaume na 6 ni wanawake.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Moshi, Mhe. Dkt. Lillian Mongella akizungumza na wazee wanaoishi kituo cha kulele wazee wasiojiweza kilichopo Kata ya Njoro Manispaa ya Moshi Mkoa wa Kilimanjaro wakati walipo kwenda kufanya matendo ya huruma. Ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani tarehe 8 Machi, 2023.  


Naibu Msajili Mahakama Kuu Kanda ya Moshi, Mhe. Sekela Mwaiseje akizungumza na wazee wanaoishi kituo cha kulele wazee wasiojiweza kilichopo Kata ya Njoro Manispaa ya Moshi Mkoa wa Kilimanjaro wakati walipo kwenda kufanya matendo ya huruma. Ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani tarehe 8 Machi, 2023.  

Sehemu ya wazee wanaoishi kituo cha kulele wazee wasiojiweza kilichopo Kata ya Njoro Manispaa ya Moshi Mkoa wa Kilimanjaro.

Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya Moshi Mhe. Oppotuna Kipeta akimkabidhi zawadi mmoja wa wazee katika kituo cha Njoro Moshi.

Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Moshi Bi. Maria Itala akiwa amebeba sehemu ya zawadi za matendo ya huruma.





Hakuna maoni:

Chapisha Maoni