Na Mwandishi Wetu-Mahakama, Dar es Salaam
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Mhe. Monica Otaru jana tarehe 8 Machi, 2024 amewaongoza watumishi wanawake wa Mahakama hiyo kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani kwa njia ya aina yake.
Watumishi hao walipatiwa mafunzo maalum na maafisa kutoka Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Watumishi wa Umma (PSSSF) na Madaktari Bingwa wa Matatizo ya Wanawake kutoka HospitalI ya Palestina Sinza.
Afisa kutoka NHIF aliwaeleza watumishi jinsi Mfuko huo unavyofanya kazi, taratibu zake na gharama mbalimbali.
Naye Daktari kutoka NHIF alieleza namna taasisi yake inavyoshirikiana nao katika kukamilisha huduma za kimatatibabu, ikiwa pamoja na aina ya matibabu na hatua za kuweza kufanikisha kwa taratibu zilizopangwa.
Pia watumishi walipata nafasi ya kusikiliza na kuelezwa juu ya saratani zinazoumiza na saratani zinazowasumbua wanawake.
Walipatiwa mafunzo namna saratani inavyopatikana, sababu zinazopelekea saratani na jinsi ya kujikinga na magonjwa ya saratani.
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Mhe. Monica Otaru (kushoto) akizungumza na Watumishi Wanawake wa Mahakama hiyo (hawapo kenye picha). Kulia ni Mtendaji wa Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Bi. Anita Kabwogi.
Afisa kutoka NIHF na picha chini ni Daktari kutoka mfuko huo.
Daktari Bingwa.
Afisa kutoka Mfuko wa PSSSF.
Watumishi wa Mahakama hiyo wakimsikiliza mmoja wa maafisa kutoka NHIF. Picha chini wakiwa katika picha ya pamoja.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni