Na Stephen Kapiga-Mahakama Mwanza.
Watumishi Wanawake wa Mahakama ya Tanzania mkoani Mwanza wameungana na wanawake wenzao Duniani katika kuadhimisha kilele cha siku ya Wanawake jana tarehe 08 machi 2024 kilele cha siku hiyo kilichofanyika kimkoa wilayani Misungwi.
Maadhimisho hayo, yaliyobeba kauli mbiu isemayo “Wekeza kwa Mwanamke kuharakisha maendeleo ya Taifa na ustawi wa jamii” yalihudhuliwa na watumishi wanawake mbalimbali kutoka taasisi za Serikali na binafsi.
Akihutubia wakati wa maadhimisho hayo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Amos Makala amewasihi Wanawake kupaza sauti zao hasa pale wanapoona vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake wenzao ili kuweza kufikia malengo ya kauli mbiu hiyo ya mwaka huu.
“wengi wamekuwa wakifikiri kuwa ukatili wa kijinsia ni mpaka waone mwanamke amejeruhiwa au kupigwa lakini ukatili wa kijinsia unaenda mbali zaidi ya hapo kwani hata vitendo tu vya kumshusha hadhi mwanamke navyo ni mojawapo wa ukatili wa kijinsia hivyo msikae kimya mara vitendo hivyo vitendwapo dhidi ya mwanamke ili kuweza kufikia lengo la maendeleo ya taifa na ustawi wa jamii kwa ujumla,” alisema Mhe. Makala.
Katika kuadhimisha siku hiyo, wanawake hao wa Mahakama za Mjini Mwanza waliweza pia kutoa misaada ya kijamii kwa kituo cha kulelea Watoto yatima kiitwacho Hisani Makao ya Watoto kilichopo Wilayani Ilemela jijini Mwanza ambapo walitoa vitu mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya Watoto waishio katika kituo hicho.
Pia,
katika kuhitimisha kilele hicho wanawake hao kwa pamoja walikutana na
kupongezana kwa kupeana zawadi na pia kufanya tafrija fupi katika viwanja vya
Otto Longoue iliyopo wilayani Misungwi katika Kata ya Usagara tukio lililofana
na kuwavutia wanawake wengi na hata baadhi ya wanaume na hivyo kuwapongeza kwa
kuonesha ushirikiano wao kwa vitendo.
Naibu Msajili
Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza Mhe. Cresensia Kisongo akiwaongoza
watumishi wanawake wa Mahakama ya Tanzania Kanda ya Mwanza kuingia katika
viwanja vya Halmashauri ya Misungwi wakati wa maadhimisho ya kilele cha siku ya
wanawake Duniani kimkoa ilifanyika wilayani Misungwi mkoani Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza
Mhe. Amos Makala akihutubia sehemu ya wanawake (hawapo pichani) waliojitokeza
katika kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani maadhimisho
yalifonyaika Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza.
Baadhi ya
watumishi wakiwa katika picha ya pomoja na mezaa kuu (waliokaa katika viti
wakiongozwa na Jaji wa Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Mwanza Mhe Lilian
Itemba wa tau kutoka kulia kwa walioketi) wakati wa tafrija fupi iliyofanyika
katika viwanja vya OTTO LONGOUE mara baada ya kumaliza kilele cha siku ya Mwanamke
Duniani liyofanyika Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza.
Jaji wa Mahakama Kuu
ya Tanzania Kanda ya Mwanza, Mhe. Lilian Itemba (wapili kutoka kulia) akiwa pamoja
na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza Mhe.Cresensia
Kisongo pamoja na Mhe. Veronica Mugendi (wa pili kutoka kushoto) na Mhe.
Tumsifu Barnabas (wa kwanza kutoka kushoto) wakiwa tayari kwa ajili ya tafrija
ya kupongezana wanawake tafrija iliyofanyika katika viwanja vya OTTO LONGOUE.
Sehemu ya Wanawake
ambao ni watumishi wa Mahakama ya Tanzania mkoani Mwanza wakilisakata Rhumba
wakati wa tafrija fupi iliyofanyika katika viwanja vya OTTO LONGOUE katika
kuadhimisha siku ya mwanamke Duniani.
Sehemu ya wanawake ambao ni watumishi wa Mahakama ya Tanzania katika mkoa wa Mwanza wakifuatilia kwa makini hotuba iliyokuwa ikitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Amos Makala wakati wa kilele cha siku ya wanawake Duniani iliyofanyika kimkoa Wilayani Misungwi.
Sehemu ya wanawake
watumishi wa Mahakama zilizopo jijini Mwanza wakiwa katika kituo cha kulelea
Watoto yatima cha Hisani Makao ya Watoto walipopeleka misaada mbalimbali ya
kijamii kwa Watoto waishio katika kituo hicho.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni