Jumanne, 12 Machi 2024

TANZIA; MTUMISHI WA MAHAKAMA YA WILAYA KONDOA AFARIKI DUNIA

Bi. Annastazia John Massawe enzi za uhai wake.

TANZIA

Mahakama ya Tanzania inasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa Mtumishi wake Bi. Annastazia John Massawe aliyekuwa akihudumu Mahakama ya Wilaya Kondoa iliyopo mkoani Dodoma kama Mwandishi Mwendesha Ofisi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo tarehe 12 Machi, 2024 na Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dodoma, Bw. Sumera Manoti mtumishi huyo amefariki leo tarehe 12/03/2024 akiwa Mkoani Kilimanjaro alipokuwa akipatiwa matibabu.

Bw. Manoti amesema kuwa mipango ya mazishi inaratibiwa na familia ya marehemu kwa kushirikiana na Uongozi wa Mahakama na mazishi yanatarajiwa kufanyika wiki hii huko Kibosho Mkoani Kilimanjaro.

Mahakama ya Tanzania inaungana na ndugu, jamaa na marafiki kuomboleza msiba huu mzito wa kuondokewa na mpendwa wetu.

BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni