WATUMISHI WANAWAKE MAHAKAMA YA RUFANI WAFANYA MATENDO YA HURUMA GEREZANI SEGEREA
Na Magreth Kinabo -Mahakama
Mkurugenzi Msaidizi kutoka Kurugenzi ya Usimamizi wa Mashauri wa Mahakama ya Tanzania,na Naibu Msajili Mhe. Hawa Mnguruta amewaasa mahabusu wanawake katika gereza la Segerea kutumia fursa hiyo ya kuwa gerezani kujirekebisha kitabia ili waweze kuwa raia wema.
Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi huyo, akiwa amewakilisha ya majaji wanawake wa Mahakama ya Rufani Tanzania, wakati baadhi ya watumishi wa Mahakama hiyo walipokwenda gereza la mahabusu la Segerea kwa ajili ya kutoa zawadi za sabuni, taulo za kike na maziwa ya watoto kwa mahabusu ya wanawake ikiwa ni hatua ya kuwapa faraja kwenye kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani.
“Ningependa nichukue nafasi hii kwa niaba ya wengine kuwa lengo letu la kufika mahali hapa ni kushirikiana nanyi katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani, ili kuwapa moyo na faraja katika mazingira magumu mliyonayo,” alisema Mhe.Mnguruta.
Mhe. Mnguruta aliwaomba wanawake hao wasikate tamaa bali wachukue kuwepo kwao gerezani hapo kuwa ni nafasi ya mafunzo ya urekebishaji wa tabia.
Kwa upande wake Mkuu wa Sehemu ya wanawake katika gereza la Mahabusu Segerea, Hamida Matimba, aliwashukuru watumishi hao kwa moyo huo wa kujitolea na kuwajali wengine.
Baadhi ya Watumishi wanawake wa Mahakama ya Rufani Tanzania wakiwa katika Gereza la Segerea walipoenda kutoa zawadi kwenye gereza la wanawake ikiwa ni hatua ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani.
Picha ya juu na chini Mkuu wa Sehemu ya wanawake katika gereza la Mahabusu Segerea, Hamida Matimba akitoa maelezo mafupi ya gereza hilo kwa watumishi hao.
Mkurugenzi Msaidizi kutoka Kurugenzi ya Usimamizi wa Mashauri wa Mahakama ya Tanzania,na Naibu Msajili Mhe. Hawa Mnguruta akikabidhi zawadi za taulo za kike na sabuni kwa Mkuu wa Sehemu ya wanawake katika gereza la Mahabusu Segerea, Hamida Matimba,ambaye amewakilisha ya Majaji wanawake wa Mahakama ya Rufani Tanzania (kulia)ikiwa ni ishara ya kuwapa faraja mahabusu wanawake katika kusherekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani wakati watumishi hao walipokwenda kutoa zawadi hizo.
Mkuu wa Sehemu ya wanawake katika gereza la Mahabusu Segerea, Hamida Matimba akimshukuru Mkurugenzi Msaidizi kutoka Kurugenzi ya Usimamizi wa Mashauri wa Mahakama ya Tanzania,na Naibu Msajili Mhe. Hawa Mnguruta baada ya kukabidhiwa zawadi hizo.
Baadhi ya Watumishi wa Mahakama ya Rufani Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutoka kwenye gereza la Mahabusu la Segerea kwa ajili ya kutoa zawadi kwenye gereza la wanawake ikiwa ni hatua ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni