Na. Mwinga Mpoli – Mahakama, Mbeya
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya Mhe. Dunstan Ndunguru
amewahimiza watumishi wa Mahakama katika kanda hiyo kufanya kazi kwa uadilifu
kwa kuzingatia maadili na weledi.
Ameyasema
hayo jana tarehe 02 Aprili, 2024 alipokuwa kwenye ziara ya kikazi kukagua
shughuli mbalimbali za kimahakama katika Mahakama ya Wilaya Songwe.
Mhe.
Ndunguru alitoa rai kwa watumishi kufanya kazi kwa ushirikiano baina yao na
wadau wengine wa Mahakama ili kuhakikisha kazi hazikwami na haki inatolewa kwa
wakati.
“Nawapongeza
sana kwa jitihada kubwa mnayofanya katika usikilizaji wa mashauri hasa
ukiangalia kazi kubwa ya Mahakama ni kusikiliza Mashauri. Nimesikiliza taarifa ya
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Songwe na kuona taarifa ya
masahuri inashabihiana na kasi ya usikilizaji wa mashauri...
Aidha,
mifumo yetu ya usimamizi wa mashauri haidanganyi ipo wazi inabainisha ni kwa namna
gani mna kasi ya usikilizaji wa mshauri. Tuendelee kuwahudumia wateja wetu kwa
uadilifu na weledi” alisema Jaji Ndunguru.
Katika
ziara hiyo pia, Mhe. Ndunguru alipata fursa ya kutembelea Mahakama ya Mwanzo
Udinde iliyopo katika Kata ya Kapalala Wilayani Songwe.
Kwa
upande wake, Mtendaji wa Kata ya Kapalala wilayani Songwe Bw. David Joseph
Haule alieleza namna gani uwepo wa Mahakama hiyo ulivyowasaidia wananchi
kupunguza uhalifu na kusaidia kudumisha amani na utengamano.
Akisoma
taarifa ya utendaji kazi wa Mahakama ya Willaya Songwe, Hakimu Mkazi Mfawidhi
wa Mahakama ya wilaya Songwe Mhe. Augustine Lugome alisema, kituo cha Mahakama
ya Mwanzo Udinde kipo umbali wa kilometa 80 kutoka Mahakama ya Wilaya kinapokea
mashauri mengi na kinafanya vizuri kiutendaji.
“Hali
za watumishi, usimamizi wa mashauri, matumizi ya mifumo ya ki-TEHAMA (e-CMS na
PCMA), utoaji wa nakala za hukumu na mienendo ya mashauri unaendelea kuimarika,
vilevile usalama wa majengo na viwanja vya Mahakama katika wilaya upo salama,”
aliongeza Mhe. Lugome katika taarifa yake
Katika
ziara hiyo Mhe. Nduguru aliambatana na Naibu Msajili Mfawidhi Mahakama Kuu
Kanda ya Mbeya Mhe. Aziza Temu, na Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Bi.
Mavis Miti.
Jaji Mfawidhi wa
Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Mhe. Dunstan Ndunguru akisaini Kitabu katika kituo
cha Mahakama ya Mwanzo Udinde kabla ya kuanza ukaguzi.
Jaji Mfawidhi wa
Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Mhe. Dunstan Beda Ndunguru wa tatu kulia akiwa kwenye picha ya pamoja na sehemu ya watumishi Mahakama ya Wilaya Songwe. Wengine ni Naibu Msajili Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Mhe. Aziza Temu (wa tatu kushoto), Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya
Bi Mavis Miti (wa pili kulia) na Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya
Songwe Mhe. Augustine Lugome.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Mhe. Dunstan Ndunguru wa kwanza kulia akikagua na kuzungumza na wananchi katika moja ya viwanja vya Mahakama katika Wilaya Songwe kilichopo Kata ya
Kapalala.
Jaji Mfawidhi wa
Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Mhe. Dunstan Ndunguru wa tatu kulia akiwa kwenye picha ya pamoja na ujumbe alioambatana nao alipotembelea Ofisi ya Mtendaji Kata ya Kapalala.
Mtendaji wa Kata ya Kapalala wilayani Songwe Bw. David Joseph Haule akieleza jambo wakati alipotembelewa ofisini kweke Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Mhe. Dunstan Ndunguru.
(Habari Hii imehaririwa na Innocent Kansha - Mahakama)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni