Jumatano, 3 Aprili 2024

RAIS SAMIA ATEUA JAJI MAHAKAMA KUU

  • Yumo pia Msajili Mkuu, Msajili Mahakama Kuu

Na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Msajili wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Silyvester Joseph Kainda kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo tarehe 3 April, 2024 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bi. Zuhura Yunus, Rais Samia pia alimteua Mhe. Eva Kiaki Nkya kuwa Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania. 

Kabla ya uteuzi wake, Mhe. Nkya alikuwa Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma ya Sheria katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Aidha, taarifa hiyo inaonyesha kuwa Rais Samia pia amemteua Mhe. Chiganga Mashauri Tengwa kuwa Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania. MheTengwa alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya TanzaniaKanda ya Geita.


Mhe. Silyvester Joseph Kainda.


Mhe. Eva Kiaki Nkya.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni