Alhamisi, 2 Mei 2024

JAJI KIONGOZI APANDA MTI KATIKA KITUO JUMUISHI CHA UTOAJI HAKI DODOMA

Na Arapha Rusheke-Mahakama Kuu, Dodoma

Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Mohamed Siyani   amewaongoza Majaji na Viongozi wengine kwenye zoezi la upandaji miti ndani ya eneo la Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Dodoma ikiwa ni mwendelezo wa utekelezaji wa azimio la mazingira.

Akizindua zoezi hilo leo tarehe 2 Mei 2024, Mhe Siyani aliwashi Majaji pamoja na watumishi wote kuwa na kawaida ya kupenda mazingira. “Hakikisheni zoezi hili linaenda kwa Mahakama nyingine pia,lisiishie hapa,” alisema.

Majaji wengine walioshiriki katika zoezi hilo la upandaji miti ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma, Mhe. Dkt. Juliana Masabo, Mhe. Dkt. Fatma Rashid Khalfan, Mhe. Edwin Kakolaki na Mhe. Dkt Evaristo Longopa na Mhe. Irene Musokwa.

Viongozi wengine walioshiriki ni Naibu Wasajili wa Mahakama Kuu, Mhe. Silivia Lushasi na MheUpendo Ngitiri na Mtendaji wa Mahakama Dodoma, Bw. Sumera Manoti.


Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Siyani akipanda mti katika Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Dodoma leo tarehe 2 Mei 2024.

Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Siyani akiongea neno baada ya kupanda mti huo.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma, Mhe. Dkt. Juliana Masabo akipanda mti katika Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Dodoma leo tarehe 2 Mei 2024.

Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, Mhe. Dkt. Fatma Rashid Khalfan  akipanda mti katika Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Dodoma leo tarehe 2 Mei 2024.

Jaji  wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, Mhe. Edwin Kakolaki  akipanda mti katika Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Dodoma leo tarehe 2 Mei 2024.

Jaji  wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, Mhe Dkt. Evaristo Longopa akipanda mti katika Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Dodoma leo tarehe 2 Mei 2024.

Jaji  wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, Mhe Irene Musokwa  akipanda mti katika Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Dodoma leo tarehe 2 Mei 2024.

Naibu Msajili Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, Mhe. Silivia Lushasi akipanda mti katika Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Dodoma leo tarehe 2 Mei 2024.

Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, Bw. Sumera Manoti akipanda mti katika Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Dodoma leo tarehe 2 Mei 2024.

(Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dar es Salaam)

 

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni