Na Eva Leshange- Mahakama, Singida
Jumla ya
mashauri tisa (9) yanatarajiwa kumalizwa katika kikao cha mwezi mmoja cha kusikiliza
mashauri ya jinai mkoani Singida ikiwa ni kikao cha kwanza kwa mwaka 2024.
Katika
taarifa ya ufunguzi iliyosomwa leo tarehe 06 Mei, 2024 na Naibu Msajili wa
Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma Mhe, Sylivia Lushasi ameeleza kuwa, jumla ya mashauri tisa
(9) ya jinai yanatarajiwa kushughulikiwa ndani ya mwezi mmoja kuanzia tarehe leo
hadi tarehe 04 Juni, 2024 na kuongeza kwamba, Mashauri 06 yanatoka Singida, shauri moja (01)
Manyoni na Iramba mashauri mawili (02).
“Sambamba
na taarifa hii, Mkoa wa Singida una mashauri 31 ambayo yanasubiri kusikilizwa
(uncauselisted) ambapo Mahakama ya Hakimu Mkazi Singida kuna mashauri 16,
Iramba 08 na Manyoni 07,” amesema Mhe. Lushasi.
Mhe.
Lushasi amebainisha kuwa mashauri tajwa hayahusishi mashauri yanayosubiri
washtakiwa kusomewa kwa mara ya kwanza (plea taking).
Aidha, amewashukuru
Wadau kwa ushirikiano wanaouonesha na kuomba umoja na mshikamano uendelee kwani
vikao hivi vimekuwa vikifanikiwa kwa kiasi kikubwa na kufikia malengo.
Naye, Jaji
Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dodoma, Mhe. Dkt Juliana Masabo amewapongeza Wadau
kwa ushirikiano ambao wamekuwa wakiuonesha katika kufanikisha usikilizwaji wa
mashauri na kuendelea kusisitiza Mawakili
na Wadau kunyumbulika (flexibility), kusoma majalada vizuri na kuongea na
wateja wao vizuri.
Vilevile
amewasisitiza Magereza kuhakikisha Mahabusu ambao wako mbali kuwa wanafikishwa
mapema angalau wiki moja kabla ya kikao kuanza ili waweze kupata muda wa kuzungumza
na Mawakili wao.
Hata hivyo, Wadau kwa pamoja wamehaidi kuendelea kutoa ushirikiano mkubwa na wamejipanga vizuri hasa Ofisi ya Mashtaka wameomba vikao vifanyike mara kwa mara kwani kwa sasa wana bajeti ya kutosha kuwezesha mashahidi.
Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, Mhe. Dkt. Juliana Masabo (kushoto) akielezea jambo katika kikao cha kusikiliza mashauri ya jinai mkoani Singida. Aliyeketi kushoto kwa Jaji Mfawidhi ni Naibu Msajili Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dodoma, Mhe. Sylivia Lushasi.
Mwakilishi kutoka Gereza la Wilaya Singida, Bw.Lakwanti akitoa taarifa fupi katika kikao hicho.
Naibu
Msajili Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, Mhe.Sylivia Lushasi akifafanua jambo
katika kikao





Hakuna maoni:
Chapisha Maoni