Jumatatu, 8 Julai 2024

JAJI LUVANDA, KATIBU MKUU KATIBA NA SHERIA WATEMBELEA BANDA LA MAHAKAMA SABASABA


Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Elinaza Luvanda akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi lililopo ndani ya banda kuu la Mahakama ya Tanzania katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), 2024 yanayoendelea kufanyika katika uwanja wa Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa Temeke jijini Dar es Salaam. Mhe. Luvanda alitembelea banda hilo jana tarehe 07 Julai, 2024.

 Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya ushiriki wa Mahakama katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), 2024, Mhe. Hussein Mushi (kushoto) akimueleza jambo Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Ardhi, Mhe. Elinaza Luvanda (wa pili kushoto kwake).
Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Bi. Mary Makondo (kushoto) akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki (EACJ) lililopo ndani ya banda la Mahakama kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), 2024. Bi Mary alitembelea banda la Mahakama jana tarehe 07 Julai, 2024.
 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Bi. Mary Makondo akiwa katiba mabanda mbalimbali alipotembelea banda la Mahakama ya Tanzania jana tarehe 07 Julai, 2024 lililopo kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni